Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo

Na Woinde Shizza,Arusha

Jeshi la polisi mkoani hapa linamshikilia mwanafunzi wa  Mwaka wa tatu  wa chuo cha maendeleo  ya jamii .Tengeru  aliyejulikana kwa jina la  Harold Mmbando (23)  mkazi wa Arusha kwa kosa la kutoa taarifa za uchochezi dhidi ya Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein na Mkuu wa majeshi Davis  Mwamunyange  pamoja na kusambaza ujumbe wa maneno makali juu ya viongozi hao.

Akiongelea  tukio kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Charles Mkumbo  alisema kuwa tukio hilo lilitokea Mei 17 mwaka huu majira ya saa 09:00  asubuhi .

Alisema kuwa mwanafunzi huyo alitoa taarifa za uchochezi kuhusu mkuu wa majeshi  ambapo alimtaka mkuu huyo wa majeshi kupindua nchi na kusema kuwa haiwezekani viongozi wote wawe  nje ya nchi huku hakuna kiongozi aliyepewa mamlaka ya kukikaimu kiti.

“mtuhumiwa huyo aliandika maneno haya ,Mwamunyange pindua nchi haiwezekani wote wawe nje halafu hakuna aliyepewa mamlaka ya kukalia kile kiti,hayo ndio maneno aliyoyasema mtumiwa huyo “alisema Mkumbo.

Aidha aliongeza kuwa mbali na maneno hayo pia mtuhumiwa huyo  alisambaza ujumbe  mwingine wenye maneno yafuatayo,”Dr Shein akiuawa kama Karume sitashangaa wala kustuka naomba mungu mauaji ya kisiasa yaliyotokea Zanzibar yawe kwa viongozi wa kisasa hasa watawala na sio wananchi wa kawaida”hayo ndio maneno aliyoyaandika mtuhumiwa huyo kupitia  mitandao ya kijamii kama faccebook.

Mkumbo  alisema kuwa mtuhumiwa huyo atafikishwa mahakamani pindi tu upelelezi utakapo kamilika,huku akitoa  rai kwa watu wote wanaotumia mitandao ya kijamii kutumia mitandao hiyo  ya kijamii pasipo kukiuka sheria  na taratiu za kisheria .Alitumia muda huo pia kutoa onyo kali kwa yoyote atakaye bainika  anatumia mitandao vibaya na kusema kuwa  atachukuliwa hatuakali za kisheria  dhidi yake.

Wakati hayo yakiendelea mshtakiwa  wa kesi ya kumtukana Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania  John Pombe Magufuli Isaac Emily (40),  mkazi wa Olasiti jiji  hapa  inatarajiwa kuanza kusikilizwa mfululizo kuanzia Juni 5 mwaka huu katika mahakama ya hakimu mkazi Arusha.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...