Mbunge wa zamani wa Kigoma kusini (NCCR-MAGEUZI), David Kafulila ameshindwa kwenye kesi yake iliyokuwa ikisikilizwa mahakama kuu kanda ya Tabora kuhusu kupinga matokeo yaliyompa ushindi mbunge wa CCM, Hasna Mwilima (pichani).
Kesi hii ilifunguliwa katika mahakama kuu kanda ya Tabora na kuendeshwa chini ya Jaji Ferdinand Wambari.
Katika kesi hio upande wa mlalamikaji (Kafulila) uliongozwa na mawakili Prof. Abdallah Safari, Tundu Lissu na Daniel Lumenyera, Ili hali upande wa mlalamikiwa (Husna) uliongozwa na wakili Kenedy Fungamtama pamoja na mawakili wa serikali upande wa mwanasheria mkuu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...