• Tshs 10,000 kwa mfuko wa 50Kg Dar-esSalaam
• Bei kushushwa nchi nzima ambapo Saruji ya Dangote inauzwa
• Punguzo la zaidi ya asilimia 20 ya bei ya saruji Tanzania
Kampuni baba ya saruji, Dangote Cement imepunguza bei ya saruji yake ili kuongeza ushindani kwenye soko la saruji Tanzania. Alhaj SadaLadan-Baki, Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Dangote amesema bei ya saruji yao aina ya 32.5R imeshuka mpaka kufikia shilingi za kitanzania 10,000 kwa mfuko wa kilo 50 wa saruji, wakati saruji ya 42.5R ikiishuka mpaka shilingi za kitanzania 10,500 kwa mfuko wa kilo 50 kutoka kiwandani mpaka popote uliko Dar es Salaam. Usafiri ni bure!

“Tunatambua uhitaji mkubwa wa miundo mbinu bora, na moja ya njia ya kulikabili tatizo hili ni kumfanya kila mtanzania kuweza kuwa na uwezo wa kununua rasilimali za ujenzi kwa kuweka bei mbadala kwa kila mtanzania,” alisisitiza. Uwekezaji wa zaidi dola za kimarekani milioni 600 utaongeza kasi ya ukuaji na uboreshaji wa miundo mbinu, ajira na kuisaidia serikali katika jitihadi zake za kukuza uchumi wa nchi. Dangote Cement.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...