Assalaam Aleikhum,
Updates za familia ya Ankal Issa Michuzi iliyopatwa na msiba wa kuondokewa na Mtoto wa Ankal, Maggid Muhidin (18),  aliyefariki Jumapili Mei 8, 2016 huko Durban, Afrika Kusini, alikukuwa masom0ni:

Mwili wa Marehemu umeshawsili  nchini jana Ijumaa Mei 13, 2016 majira ya saa tisa  mchana kwa  ndege ya shirika la Emirates kupitia Dubai (kwa kukosekana kwa  ndege za moja kwa moja kuja nchini kutoka Durban). 
Mwili wa kijana wetu umepokelewa na wazazi, ndugu, jamaa, majirani na marafiki katika   uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius  Nyerere eneo la Cargo la Swissport, Jijini Dar es salaam.
Mazishi yamepangwa  kufanyika leo  Jumamosi saa 10  alasiri katika Makaburi ya Kisutu jijini Dar es salaam. Taratibu  za kuandaa mazishi zitaanza  saa 4 asubuhi leo  Jumamosi, nyumbani  kwa mama wa marehemu kota za Wazo Hill, Tegeta, ulipo msiba.
 Jeneza lenye mwili wa marehemu Maggid baada ya kuwasili Dar es salaam jana Ijumaa
Ankal akiwa na ndugu, jamaa, marafiki na badhi ya viongozi wa msikiti mara baada ya kuwasili na mwili wa marehemu katika msikiti wa Maamur, Upanga, Dar es salaam, ambako unahifadhiwa hadi baadae leo kabla ya kupelekwa Wazo Hill saa nne kwa dua na baadaye kurudi hapo msikitini kuswaliwa na hatimaye kupelekwa makaburi ya Kisutu kwa mazishi saa 10 Alasiri.


Ankal akiwa na ndugu, jamaa na  marafiki mara baada ya kuwasili katika msikiti wa Maamur, Upanga, Dar es salaam

Ankal akiwa msibani Wazo Hill na wanahabari wenzie usiku huu. Kutoka kushoto ni Faraja Mugwabati, Maggid Mjengwa na Sufiani Mafoto.
NAMNA YA KUFIKA MSIBANI
Ukitokea Tegeta Kibaoni kama unaelekea Kiwanda cha Cement cha Wazo Hill, mbele mkono wako wa kulia kuna Kanisa la KKKT na ukienda mbele tena kidogo, utaona Bar yenye uzio wa rangi ya njano ambao umeandikwa "Twiga Cement",  hapo pana bango linaloelekeza njia karibu na kituo cha Bajaji nje. Unaingia upande huo wa kulia mita 250 mbele unakata tena kulia, mita 70 mbele utakuta maturubai, ndipo msibani.
Innalillah wa inna ilayhi raajiun
-AMIN.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 45 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 09, 2016

    Pole sana Uncle Michuzi m/mungu awape wepesi katika msiba huu mzito. Mungu ailaze roho ya marehem mahala pema peponi Amin.

    ReplyDelete
  2. inalilah wainailayhi rajiun. Poleni wafiwa esp Uncle.

    Allah amuondolee adhabu ya kaburi, ampe kauli dhabit mbele yake nyuma yetu, amin amin amin

    ReplyDelete
  3. Polenisana Brother Michuzi

    Mungu awape nguvu kipindi hiki kigumu

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 09, 2016

    Pole nyingi kwa familia ya Michuzi

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 09, 2016

    La! Pole sana Ancle na familia nzima.

    ReplyDelete
  6. RIP MAGGID,POLE SANA ANKAL MICHUZI!

    ReplyDelete
    Replies
    1. AnonymousMay 10, 2016

      Dah! Nilifikiri Maggid Mjengwa. RIP Maggid. We are right behind you!

      Delete
  7. Poleni sana kwa msiba kaka Michu na familia. Mungu awatie nguvu katika kipindi hiki kigumu.

    ReplyDelete
  8. Poleni sana Uncle Michuzi kipindi cha giza nene...

    ReplyDelete
  9. Poleni wafiwa mola amempenda zaidi

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 10, 2016

    Nawapa pole wafiwa wote. MOLA amrehemu ndugu yetu apumzike kwa amani. AMINA.

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 10, 2016

    R.I.P. Maggid.
    Poleni sana familia ya Michuzi. Mungu awape nguvu katika kipindi hiki kigumu

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 10, 2016

    Pole sana Uncle Michuzi na familia nzima. Mwenyezi Mungu awape nguvu katika kipindi hiki kigumu.

    ReplyDelete
  13. Ina Lillah Waina Illah Rajughun. Pole Bwana Michuzi Mungu amuwqekwe mahala pema peponi bwana mdogo.

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 10, 2016

    Pole sana kaka Michuzi. mshukuru mungu kwa matendo yake makuu. Jina la bwana libarikiwe.

    ReplyDelete
  15. Pole sana Maggid kwa msiba wa mwanao, Mwenyezi Mungu akupe wepesi wakat huu mgumu wa majonzi.

    ReplyDelete
  16. Inalilah Wainailayhi Rajiun. Poleni sana Allah awape subra katika kipindi hiki kigumu

    ReplyDelete
  17. AnonymousMay 10, 2016

    'Ina lillah wainaillahih rajiuun'. Hakika sisi ni waja wa allah na kwake tutarejea. Bila shaka safari hii ni ya wote ukiwa mume, mke, tajiri , masikini na kabila ama taifa lolote lile.

    Hapa ukitafakari siono sababu ya mwanaadamu kubaguana kwa kisingizio chochote kile.Mola alituumba makabila kwa makabila, mataifa kwa mataifa ili tupate kujuana.

    Ankal na familia yako huu ndio usia wangu kwako, subira ndio mtihani wetu sote, twamuombea kwa allah ailaze roho ya mpendwa wako mahali pema peponi na kwa wale wote walio fika mbele ya haki "AMIN"

    Tupo pamoja kama ndugu, Allah ndie mjuzi.

    ReplyDelete
  18. AnonymousMay 10, 2016

    Pole sana Ankal! Mungu awape nguvu katika wakati huu mgumu.

    ReplyDelete
  19. AnonymousMay 10, 2016

    Pole sana Ankal, hakika kila nafsi itaonja MAut, na hakuna kitakachobaki ila ALLAH, msiba mzito wa mtoto mwenye ez Mungu awajaalie faraja wewe na mwenza wako na wote waloguswa na msibaa huu,

    INNA LILLA WA INNA ILAIHI RAAJIUUN

    ReplyDelete
  20. AnonymousMay 10, 2016

    Poleni familia ya Michuzi kwa kupoteza kijana wenu.

    ReplyDelete
  21. Poleni sana kwa Msiba huu Mkubwa,MUNGU awape nguvu na faraja katika kipindi hiki kigumu!!

    ReplyDelete
  22. Ally AbdallahMay 10, 2016

    إنا لله وإنا إليه راجعون
    Inna lilahi wainna ilayhi raajiun

    Poleni Ankal M'Mungu awape subra na amsameh makosa yake, amlinde na ghadhabu za kabri na ampe kitabu chake kwa mkono wa kulia... Hakika msiba ni mawaidha tosha sana kwetu tuliobaki tujipange kwa kujiuliza, je, tutamuonyesha nini m'mungu tukirudi kwake baada ya haya maisha ya mpito? What difference have we made in this world?

    ReplyDelete
  23. Poleni sana wafiwa na MwenyeziMungu awazidishie subra...Mola ametoa..na Mola ametwaa.

    ReplyDelete
  24. Poleni sana kwa mcba

    ReplyDelete
  25. Pole sana Ankal Michuzi na wanafamilia wote.Roho wa Marehemu apate Rehema kwa Mungu, apumzike kwa Amani,Amen!

    ReplyDelete
  26. AnonymousMay 11, 2016

    MUNGU AWE NAWE KATIKA KIPINDI HIKI KIGUMU KAKA MICHUZI, TUMEPOTEZA KIJANA MWENYE KILA AINA YA SIFA NA MALENGO MENGI.INASIKITISHA SANA.LAKINIYOTE TUMUACHIE MUUMBA ALIYETUWEKA HAPA DUNIANI. TUKO PAMOJA KIROHO,MWENYEZI MUNGU AWE NAE DAIMA.

    ReplyDelete
  27. AnonymousMay 11, 2016

    Inna Lillahi Wainna Illaihi Rajiun, poleni sana wafiwa na msiba wa Maggid, Allah amsamehe makosa yake. Poleni sana

    ReplyDelete
  28. Kwa niaba ya Watanzania wote waliopo hapa St. Petersburg, Russia tafadhali pokeeni pole nyingi sana toka kwetu. Mbali ya distance kubwa kati yetu, mawazo na sala zetu ziko pamoja nanyi. Muumba awaongezee nguvu na faraja kyk kipindi hichi kigumu

    ReplyDelete
  29. AnonymousMay 11, 2016

    Pole sana Michuzi na familia kwa msiba huo mzito. Roho yake ipumzike kwa amani mbinguni - Amina.

    ReplyDelete
  30. AnonymousMay 11, 2016

    Poleni sana.

    ReplyDelete
  31. AnonymousMay 12, 2016

    POLENI SANA FAMILIA YA MICHUZI. RIP MAJID

    ReplyDelete
  32. AnonymousMay 12, 2016

    Inna lillahi wainna ilaihi rajiuun. Poleni sana wafiwa kwa msiba. Allah awape subra katika kipindi hiki kigumu cha msiba.

    ReplyDelete

  33. POLE SAANA MR. ISSA MICHUZI.

    MWANA JUGNU MEHU"

    ReplyDelete
  34. Ephata SozigwaMay 13, 2016

    Pole sana Michuzi na familia

    ReplyDelete
  35. pole sana kaka michuzi.m.mungu amuondolee adhabu za kaburi

    ReplyDelete
  36. Michuzi,Masha na familia yote poleni sana.
    RIP Maggid
    Pasco

    ReplyDelete
  37. Pole sana Uncle, RIP Maggid

    ReplyDelete
  38. Inna Lillahi Wainna Illaihi Rajiun...

    ReplyDelete
  39. Pole Sana ankal na Familia kwa Msiba. Mwenyezi Mungu awatie nguvu wakati wa kipindi hiki kigumu.

    ReplyDelete
  40. Innah Lillah wa Innah Illahi rajiun. Poleni Sana kwa msiba ankali Allah awapeni subra

    ReplyDelete
  41. AnonymousMay 14, 2016

    Pole sana Bwana Michuzi na familia yote kwa msiba WA mwanao. Mungu aipoke roho ya marehemu Na kuiweka mahali pema peponi, Na pia wapi with nguvu kipindi hiki kigumu ������

    ReplyDelete
  42. Pole mkuu michuzi kwa msiba wa mwanao

    ReplyDelete
  43. AnonymousMay 14, 2016

    Allah amthibishe marehem maggid

    ReplyDelete
  44. AnonymousMay 15, 2016

    Inna lillah wa inna ilayh raajiun, Mwenyezi Mungu awape subira na uvumilivu katika kipindi hiki

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...