Assalaam Aleikhum,
Updates za familia ya Ankal Issa Michuzi iliyopatwa na msiba wa kuondokewa na Mtoto wa Ankal, Maggid Muhidin (18), aliyefariki Jumapili Mei 8, 2016 huko Durban, Afrika Kusini, alikukuwa masom0ni:
Mwili wa Marehemu umeshawsili nchini jana Ijumaa Mei 13, 2016 majira ya saa tisa mchana kwa ndege ya shirika la Emirates kupitia Dubai (kwa kukosekana kwa ndege za moja kwa moja kuja nchini kutoka Durban).
Mwili wa kijana wetu umepokelewa na wazazi, ndugu, jamaa, majirani na marafiki katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere eneo la Cargo la Swissport, Jijini Dar es salaam.
Mazishi yamepangwa kufanyika leo Jumamosi saa 10 alasiri katika Makaburi ya Kisutu jijini Dar es salaam. Taratibu za kuandaa mazishi zitaanza saa 4 asubuhi leo Jumamosi, nyumbani kwa mama wa marehemu kota za Wazo Hill, Tegeta, ulipo msiba.
Jeneza lenye mwili wa marehemu Maggid baada ya kuwasili Dar es salaam jana Ijumaa
Ankal akiwa na ndugu, jamaa, marafiki na badhi ya viongozi wa msikiti mara baada ya kuwasili na mwili wa marehemu katika msikiti wa Maamur, Upanga, Dar es salaam, ambako unahifadhiwa hadi baadae leo kabla ya kupelekwa Wazo Hill saa nne kwa dua na baadaye kurudi hapo msikitini kuswaliwa na hatimaye kupelekwa makaburi ya Kisutu kwa mazishi saa 10 Alasiri.
Ankal akiwa na ndugu, jamaa na marafiki mara baada ya kuwasili katika msikiti wa Maamur, Upanga, Dar es salaam
NAMNA YA KUFIKA MSIBANI
Ukitokea Tegeta Kibaoni kama unaelekea Kiwanda cha Cement cha Wazo Hill, mbele mkono wako wa kulia kuna Kanisa la KKKT na ukienda mbele tena kidogo, utaona Bar yenye uzio wa rangi ya njano ambao umeandikwa "Twiga Cement", hapo pana bango linaloelekeza njia karibu na kituo cha Bajaji nje. Unaingia upande huo wa kulia mita 250 mbele unakata tena kulia, mita 70 mbele utakuta maturubai, ndipo msibani.
Innalillah wa inna ilayhi raajiun
-AMIN.







Pole sana Uncle Michuzi m/mungu awape wepesi katika msiba huu mzito. Mungu ailaze roho ya marehem mahala pema peponi Amin.
ReplyDeleteinalilah wainailayhi rajiun. Poleni wafiwa esp Uncle.
ReplyDeleteAllah amuondolee adhabu ya kaburi, ampe kauli dhabit mbele yake nyuma yetu, amin amin amin
Polenisana Brother Michuzi
ReplyDeleteMungu awape nguvu kipindi hiki kigumu
Pole nyingi kwa familia ya Michuzi
ReplyDeleteLa! Pole sana Ancle na familia nzima.
ReplyDeleteRIP MAGGID,POLE SANA ANKAL MICHUZI!
ReplyDeleteDah! Nilifikiri Maggid Mjengwa. RIP Maggid. We are right behind you!
DeletePoleni sana kwa msiba kaka Michu na familia. Mungu awatie nguvu katika kipindi hiki kigumu.
ReplyDeletePoleni sana Uncle Michuzi kipindi cha giza nene...
ReplyDeletePoleni wafiwa mola amempenda zaidi
ReplyDeleteNawapa pole wafiwa wote. MOLA amrehemu ndugu yetu apumzike kwa amani. AMINA.
ReplyDeleteR.I.P. Maggid.
ReplyDeletePoleni sana familia ya Michuzi. Mungu awape nguvu katika kipindi hiki kigumu
Pole sana Uncle Michuzi na familia nzima. Mwenyezi Mungu awape nguvu katika kipindi hiki kigumu.
ReplyDeleteIna Lillah Waina Illah Rajughun. Pole Bwana Michuzi Mungu amuwqekwe mahala pema peponi bwana mdogo.
ReplyDeletePole sana kaka Michuzi. mshukuru mungu kwa matendo yake makuu. Jina la bwana libarikiwe.
ReplyDeletePole sana Maggid kwa msiba wa mwanao, Mwenyezi Mungu akupe wepesi wakat huu mgumu wa majonzi.
ReplyDeleteInalilah Wainailayhi Rajiun. Poleni sana Allah awape subra katika kipindi hiki kigumu
ReplyDelete'Ina lillah wainaillahih rajiuun'. Hakika sisi ni waja wa allah na kwake tutarejea. Bila shaka safari hii ni ya wote ukiwa mume, mke, tajiri , masikini na kabila ama taifa lolote lile.
ReplyDeleteHapa ukitafakari siono sababu ya mwanaadamu kubaguana kwa kisingizio chochote kile.Mola alituumba makabila kwa makabila, mataifa kwa mataifa ili tupate kujuana.
Ankal na familia yako huu ndio usia wangu kwako, subira ndio mtihani wetu sote, twamuombea kwa allah ailaze roho ya mpendwa wako mahali pema peponi na kwa wale wote walio fika mbele ya haki "AMIN"
Tupo pamoja kama ndugu, Allah ndie mjuzi.
Pole sana Ankal! Mungu awape nguvu katika wakati huu mgumu.
ReplyDeletePole sana Ankal, hakika kila nafsi itaonja MAut, na hakuna kitakachobaki ila ALLAH, msiba mzito wa mtoto mwenye ez Mungu awajaalie faraja wewe na mwenza wako na wote waloguswa na msibaa huu,
ReplyDeleteINNA LILLA WA INNA ILAIHI RAAJIUUN
Poleni familia ya Michuzi kwa kupoteza kijana wenu.
ReplyDeletePoleni sana kwa Msiba huu Mkubwa,MUNGU awape nguvu na faraja katika kipindi hiki kigumu!!
ReplyDeleteإنا لله وإنا إليه راجعون
ReplyDeleteInna lilahi wainna ilayhi raajiun
Poleni Ankal M'Mungu awape subra na amsameh makosa yake, amlinde na ghadhabu za kabri na ampe kitabu chake kwa mkono wa kulia... Hakika msiba ni mawaidha tosha sana kwetu tuliobaki tujipange kwa kujiuliza, je, tutamuonyesha nini m'mungu tukirudi kwake baada ya haya maisha ya mpito? What difference have we made in this world?
Poleni sana wafiwa na MwenyeziMungu awazidishie subra...Mola ametoa..na Mola ametwaa.
ReplyDeletePoleni sana kwa mcba
ReplyDeletePole sana Ankal Michuzi na wanafamilia wote.Roho wa Marehemu apate Rehema kwa Mungu, apumzike kwa Amani,Amen!
ReplyDeleteMUNGU AWE NAWE KATIKA KIPINDI HIKI KIGUMU KAKA MICHUZI, TUMEPOTEZA KIJANA MWENYE KILA AINA YA SIFA NA MALENGO MENGI.INASIKITISHA SANA.LAKINIYOTE TUMUACHIE MUUMBA ALIYETUWEKA HAPA DUNIANI. TUKO PAMOJA KIROHO,MWENYEZI MUNGU AWE NAE DAIMA.
ReplyDeleteInna Lillahi Wainna Illaihi Rajiun, poleni sana wafiwa na msiba wa Maggid, Allah amsamehe makosa yake. Poleni sana
ReplyDeleteKwa niaba ya Watanzania wote waliopo hapa St. Petersburg, Russia tafadhali pokeeni pole nyingi sana toka kwetu. Mbali ya distance kubwa kati yetu, mawazo na sala zetu ziko pamoja nanyi. Muumba awaongezee nguvu na faraja kyk kipindi hichi kigumu
ReplyDeletePole sana Michuzi na familia kwa msiba huo mzito. Roho yake ipumzike kwa amani mbinguni - Amina.
ReplyDeletePoleni sana.
ReplyDeletePOLENI SANA FAMILIA YA MICHUZI. RIP MAJID
ReplyDeleteInna lillahi wainna ilaihi rajiuun. Poleni sana wafiwa kwa msiba. Allah awape subra katika kipindi hiki kigumu cha msiba.
ReplyDelete
ReplyDeletePOLE SAANA MR. ISSA MICHUZI.
MWANA JUGNU MEHU"
Pole sana Michuzi na familia
ReplyDeletepole sana kaka michuzi.m.mungu amuondolee adhabu za kaburi
ReplyDeleteMichuzi,Masha na familia yote poleni sana.
ReplyDeleteRIP Maggid
Pasco
Pole sana Uncle, RIP Maggid
ReplyDeleteInna Lillahi Wainna Illaihi Rajiun...
ReplyDeletePole Sana ankal na Familia kwa Msiba. Mwenyezi Mungu awatie nguvu wakati wa kipindi hiki kigumu.
ReplyDeleteInnah Lillah wa Innah Illahi rajiun. Poleni Sana kwa msiba ankali Allah awapeni subra
ReplyDeletePole sana Bwana Michuzi na familia yote kwa msiba WA mwanao. Mungu aipoke roho ya marehemu Na kuiweka mahali pema peponi, Na pia wapi with nguvu kipindi hiki kigumu ������
ReplyDeletePole mkuu michuzi kwa msiba wa mwanao
ReplyDeleteAllah amthibishe marehem maggid
ReplyDeleteInna lillah wa inna ilayh raajiun, Mwenyezi Mungu awape subira na uvumilivu katika kipindi hiki
ReplyDelete