Na Woinde
Shizza ,Arusha
Chama
cha wanunuzi na wauzaji wa Madini Tanzania TAMIDA kimetoa tamko la
kulaani kitendo cha uongozi wa Haliamshauri ya Simanjiro
kuwavamia
wafanyabiashara wa madini wa jijini Arusha maofisini wakiwa
wameambatana na Askari wenye silaha za moto na pingu kuwalazimisha
kulipa kodi ya tozo ya huduma ya Madini.
Akitoa
tamko hilo katika mkutano wa wafanya biashara wa Madini uliofanyika
katika Ofisi za wizara ya madini Kanda ya Kaskazini jijini hapa Makamu
mwenyekiti wa TAMIDA Thomas Munis alisema kitendo hicho hakikubaliki na
kimelenga kuwadhalilisha wafanyabiashara hao pamoja na wateja
wao.
Thomas
aliutaka uongozi wa Wilaya ya Simanjiro kukaa chini na kukubaliana
namna ya ulipaji wa tozo hiyo inayofikia kiasi cha shilingi Milioni 20
hadi 60 kwa mwaka, jambo ambalo alisema hawawezi kulipa mara mbili kwa
halimashauri ya Arusha pamoja na Halimashauri ya
Simanjioro.
"Sisi
kama wafanyabiashara hatupingi kulipa kodi yoyote ya madini ila tunachosikitishwa nacho ni hatua ya uongozi wa Simanjiro kutufuata maofisini
wakiwa na silaha za moto na pingu, kutaka tulipe kodi huduma ambayo
kimsingi tumekuwa tukilipa kila mwaka katika halimashauri ya Arusha",
Alisema Thomas.
Aidha
aliongozea kusema kuwa wao kama wafanyabiashara wa madini hawapingi
kulipa kodi yoyote inayotozwa kutokana na biashara ya madini ila
wanachopinga kodi hiyo kutozwa mara mbili kwa mwaka katika halimashauri
zote swala ambalo wameliomba serekli kupitia wizara ya madini kuingilia
kati swala hilo na kutatua mkanganyiko huo.
Wakati
huo huo afisa madini kutoka ofisi hiyo ya kanda Bwana Erick Mpesa amesema
kuwa wao kama kama wasimamizi wa madini katika kanda hii wanangoja
maafikiano ya pande zote mbili ikiwemo halmashauri ya Simanjiro pamoja
na jiji la Arusha juu ya Tozo hiyo ya huduma ya Madini.
Kwa
upande mwanasheria Jiji la Arusha Bahati Chojo amesema kuwa sheria
inaelekeza wazi kuwa kampuni yoyote inayofanya biashara ya madini
inapaswa kulipa tozo ya huduma kule ilipo ikiwemo kulipa kule ilipo
ofisi pamoja na maeneo ya matawi ya ofisi hizo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...