Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la uwezeshaji wa wananchi kiuchumi (NEEC), Bang'i  Issa akizungumza wakati wa kufungua masomo ya vijana walioshinda kurishiriki shindano la Ajira yangu Business plan Competition jjini Dar es Salaam leo.
Baadhi ya washiriki wa shindano la Ajira yangu waliohudhulia katika shindano hilo wakiwa kwenye mkutano leo jijini Dar es Salaam.

Na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.
WASHIRIKI wa shindano la kibiashara  la Ajira yangu Business  plan Competition  wameaswa kutumia  vyema fursa waliyoipata ya kupata mafunzo kwani yanaweza kubadili mitazamo yao ya kimaisha hususani katika masuala ya kujiajiri badala ya kuwa na fikra za kuajiliwa. 

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la uwezeshaji wa wananchi kiuchumi (NEEC), Bang'i Issa wakati akizungumza na washirikibwa shindano la Ajira yangu Business plan Competition jiji Daf es Salaam leo. Amesema kuwa watumie fursa hiyo kwani wao ni washindi wa awamu ya kwanza na kuwa kwenye 50 bora kati ya 831. Ni ushindi mmojawapo. 

Bang'i amesema kuwa wazingatie mafunzo watakayoyapata ili wachaguliwe kwe 20 bora na 10 bora.
 Pia amewaasa washiriki wa shindando hilo  kuwatumia vizuri wakufunzi pamoja na mkufunzi mkufunzi mkuu vizuri ili baadae wafanye  umakini vizuri katika kuboresha màandiko yao na kuyawasilisha kwaajili ya mchunjo.


 Nae  mwakilishi  kutoka ILO, Geras Shirove amesema kuwa  amewapongeza washiriki 50 wa kiendelea kushindania shindano hilo kwani washiriki wa shindano hilo walikua 831.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 23, 2016

    Ni fursa nzuri ya kuinua vijana wabunifu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...