Benki ya NMB PLC imeanza kutoa hati fungani ya NMB yenye riba ya 13% kwa yeyote mwenye nia ya kuwekeza na kupata faida nzuri. Hii ni mara ya kwanza kwa NMB kutoa hati fungani ya namna hii na inaweza kununuliwa kupitia matawi yote ya NMB au kwa mawakala wanaotambulika kwa kiasi cha chini cha shilingi 500,000 (laki tano tu). Kufunguliwa kwa hati fungani ya NMB kwa wananchi ni matokeo ya kupata kibali kutoka mamlaka ya masoko ya mitaji nchini - Capital Markets & Securities Authority (CMSA).

Wawekezaki wa hati fungani ya NMB watapata riba ya asilimia 13 kwa mwaka itakayolipwa kila baada ya miezi sita kwa miaka mitatu mpaka mwezi Juni 2019; Riba itakayotolewa itakatwa kodi ya mapato. Hati fungani ya NMB inauzika pia, na mteja anaweza kuiuza kwa mnunuaji mwingine na kupata fedha yake kabla ya kmukomaa kwa hati fungani – yaani miaka mitatu. Wawekezaji wanaweza kuiuza hati fungani hiyo kabla ya kukomaa katika soko la wazi kupitia mawakala wa soko la mitaji – kwa kufuata misingi ya soko la hisa la Dar es Salaam.

Hati fungani ya NMB itauzwa kuanzia tarehe 10 Mei, 2016 mpaka June 8 2016 na riba itaanza kulimbikizwa kuanzia tarehe hii. Kununua hati fungani ya NMB, mteja anatakiwa kutembelea tawi lolote la NMB kati ya matawi 175 nchini kote au kwa mawakala wanaotambuliwa.

Tembelea tawi na NMB kunua hati fungani hii na hakikisha umebeba viambatanishi vifuatavyo;
Fomu ya bondi iliyokamilika na kusainiwa
Nakala ya kitambulisho
Akaunti ya CDS
Kianzio cha fedha cha shilingi 500,000
Taarifa za akaunti yako ya benki.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 23, 2016

    Watanzania tuchangamkie fursa za uwekezaji/

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 23, 2016

    Sawa, sisi wa nje ya nchi, tukitaka je tutafanyaje? Tafadhali msiweke SIASA zetu, tunaomba majibu.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 23, 2016

    Wa nje tunafanyaje? How dumb? The Bank needs the money. Send it home!

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 24, 2016

    Swali la jamaa wa pili sio baya, ni wanao juwa kusema watafanyaje? sio kutuma pesa Home hilo sio jibu, Tunaomba wausika wa benk hii tupeni majibu, je twende Ubarozini kwetu au tunafanya nini?

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 24, 2016

    Wa nje kivipi tena! hakuna cha wa-nje wala ndani. Wamesema tembelea tawi lolote (yapo 175) upate hii huduma, sasa ikibidi upande ndege ili ufike kwenye moja ya haya matawi basi fanya hivyo kimya kimya tu...

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...