Wakati Serikali ya Halmashauri ya Wilaya ya Ilala ikiwa imepiga maarufu uuzaji wa bidhaa mbalimbali katika maeneo yasiyoruhusiwa katikati ya Jiji, bado wafanyabiashara ndogo ndogo hao wamekuwa wakiendelea na biashara zao katika maeneo yasiyoruhusiwa kama kamera ua Globu ya Jamii ilivyozinasa taswira hizi, Hapa ni katika viyunga vya posta jijini Dar es Salaam leo. Picha na Emmanuel Massaka.
Home
Unlabelled
WAMACHINGA WAENDELEA KUPETA KATIKATI YA JIJI LA DAR
Subscribe to:
Post Comments (Atom)






HALAFU HAWA WAMACHINGA WA HILI ENEO MLILOPIGA KWENYE HIZO MEZA ZINAZOONEKANA KABLA YA KONA HUWA WANA ROHO NGUMU SANA. NILISIMAMA KARIBU NA MEZA ZAO KUONGEA NA SIMU WAKANIFUKUZA NA KUTOA LUGHA MACHAFU KAMA VILE WANA HAKI KUKAA HAPO.WANA MANENO KWELI WALINIPOROMOSHEA MATUSI NIKAJIULIZA AAH-YUPI MWENYE HAKI YA KUSIMAMA HAPO, MIMI AU WAO WALIOWEKA MEZA ZAO HAPO KUFANYA BIASHARA? WAMEFANYA KAMA HAPO NI OFISI YAO RASMI NA WANADHANI HAKUNA WAKUWATATOA!! NADHANI KUNA MTU WANAMLIPA KUKAA HAPO NDIO MAANA WANAJIDAI!!!!
ReplyDeletemm! Ila wanaotakiwa kuondolewa ni wale wa Kariakoo na si hawa wa hapa Posta.
ReplyDeleteHawa vijana lazima wapewe maeneo rafiki ya biashara. Wawekwe kwenye vikundi na kusaidiwa kuendesha biashara zao. Wakizagaa mitaani wizi utaongezeka.
ReplyDeleteKila kukicha vijana wanakuja mijini kufanya biashara ya umachina, sio kazi ya serikali kuwatafutia maeneo ya biashara. Haijalishi ni wafanya biashara wadogo au wakubwa, wote tuandikishe biashara yetu na kuifanya kwenye sehemu salama ni halali, Serikali inachoweza kufanya ni kuwapa grace period ya kulipa kodi na kuwapatia fursa za mikopo, pedestrian pavements na vituo vya mabasi ni kwa ajili ya watembea kwa miguu na abiria!!!!
ReplyDelete