Watumishi wa Serikali 210 wameidhinishiwa mikopo nyumba yenye thamani shilingi bilioni 2.3 baada ya kukidhi vigezo vya Bodi ya Mfuko wa Mikopo ya Nyumba za Watumishi wa Serikali.

Kauli hiyo imetolewa leo mjini Dodoma na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi (pichani) wakati akiwasilisha bungeni hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka ujao wa fedha.

Alisema kuwa Serikli imekamilisha uhakiki wa maombi mapya 191  ya watumishi wa umma waliomba mkopo wa nyumba katika maeneo mbali.
Mhe. Lukuwi aliongeza kuwa kati ya maombi hayo watumishi 181 yamekidhi vigezo vya mfuko huo na yanatarajiwa kuidhimishwa mwishoni mwa mwezi huu.
Aidha , alisema kuwa Serikali kupitia Watumishi Housing Company (WHC) imeanza kujenga nyumba za kuuza kwa watumishi wa umma katika mikoa ya  Morogoro, Dar es salaam, Pwani, Tanga  na Mwanza
Mhe. Lukuvi alisema kuwa watumishi wa umma wanaotaka kununua nyumba hizo wanawaweza kupata mikopo yenye mashrti nafuu kupitia Benki za Azania , CRDB, NMB, BoA na Exim zilizoingia makubaliano na Watumishi Housing Company wanaojenga nyumba kwa ajili ya kuwauzia watumishi wa umma katika maeneo mbalimbali nchini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 22, 2016

    Huu ni mpango mzurwa kuwezesha watumishi wa umma kununua nyumba

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...