Na Dixon Busagaga wa Globu 
ya Jamii Kanda ya Kaskazini.
Mabingwa wa soka mkoa wa Kilimanjaro,Timu ya Kitayosce inataraji kuondoka jumapili hii kuelekea Singida huku ikikabiliwa na ukata .
Kamati ya kuisadia timu hiyo imeendelea kuhamasisha wadau mbalimbali wa soka hasa wale ambao ni wenyeji wa mkoa wa Kilimanjaro kujitokeza kuisadia timu hiyo kwa hali na mali ili iweze kuuwakilisha vyema mkoa wa Kilimanjaro.
Hata hivyo kamati inatoa pongezi kwa Kampuni inayosimamia uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro KIA(KADCO) kwa msaada wa awali iliyotoa huku ikiwakumbusha wadau wengine waliofikishiwa barua za ombi la msaada kwa timu hiyo kuzifanyia kazi.
Kwa sasa kamati ya kuisadia timu hiyo inakusanya michango kupitia namba za simu 0715331274 na 0746331274.
Mwenyekiti wa Chama cha soka mkoa wa Kilimanjaro,(KRFA) Godluck Mosha akizungumza wakati wa kuwaaga mabingwa wa soka mkoa wa Kilimanjaro, timu ya Kitayosce wanaojiandaa kuelekea mkoani Singida kushiriki ligi ya Mabingwa wa mikoa katika kituo hicho.
Baadhi ya wachezaji timu ya Kitayosce wakiwa katika uwanja wa Meimoria ambako waliagwa na uongozi wa Chama cha soka mkoa wa Kilimanjaro (KRFA)
Katibu wa Chama cha soka mkoa wa Kilimanjaro (KRFA) Mohamed Mussa akizungumza wakati wa kuiaga timu ya Kitaysce.
Mwenyekiti Mosha akikabidhi kiasi cha Sh Laki moja kwa nahodha wa timu ya Kitayosce kwa ajili ya kunua viatu kwa baadhi ya wachezaji wa timu hiyo.
Wachezaji wa Kitayosce wakiagana na Viongozi wa KRFA katika uwanja wa Meimorial. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 21, 2016

    Kilimanjaro sio ya Wachagga pekee. Na Waasu tumo!

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 22, 2016

    Angesema wanaishi Kilimanjaro badala ya kusema kabila

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 22, 2016

    Kweli Tanzania ya makabila siitambui. Ama kwa vile ni jirani na Kenya?

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 23, 2016

    Ni mfano wa habari isiyoeditiwa.....huwezi ukaandika hivi hata kidogo kama ni timamu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...