Katika
mpango wake wa kukutana na kuendelea na mfungo wa mwezi Ramadhani leo
Airtel kupitia Airtel FURSA imekutana bloggers na kuzungumzia mambo
mbalimbali ikiwemo VSOMO mfumo mpya unaomwezesha kijana wa kitanzania
,kupakua masomo ya ufundi stadi na kupata cheti kupitia simu yake ya
Airtel.
Akielezea VSOMO Mkurugenzi wa rasilimali watu bwana Patrick Foya alisema, ana anamatumaini kuwa VSOMO masomo ya Ufundi yanayotolewa na VETA kupitia simu za mkononi za Airtel, yatakua suluhisho kwa vijana wengi wenye ujuzi na ari ya kujifunza kufanya shughuli kwa uhakika kwani watakua wamejifunza mbinu zitakazowawezesha kuto bahatisha na kuongeza ufanisi katika kazi zao.
Nao bloggers walio hudhuria walikua na haya ya kusema, mfumo huu utaleta tija sana kwa vijana wengi ambao wako katika shughuli mbalimbali kupata muda wa kujifunza na kupata taaluma zitakazowawezesha kujiajiri, tunawapongeza Airtel kwa kuanzia mfumo huu wa masomo kupitia simu.
Aidha waliongeza kwa kusema wao watakuwa mstari wa mbele kushirikiana na Airtel kwa kuwafikia makundi mbalimbali ya vijana katika maeneo yao ya kazi ili kuhakikisha wanaitumia vyema fursa hii katika kujiendeleza kitaaluma.

Mkurugenzi wa rasilimali watu wa Airtel, bwana Patrick Foya akiitambulisha kwa blogger VSOMO mfumo mpya unaomwezesha kijana wa kitanzania ,kupakua masomo ya ufundi stadi yanayotolewa na VETA kupitia simu yake ya Airtel.
Mmimiliki wa 80/20 blog Shamimu akiuliza swali mara baada ya kupata ufafanuzi juu ya mpango wa VSOMO ushirikiano kati Airtel na VETA kwenye mkutano ulifatiwa na Futari.
Mzee John kitime (katikati) wakijadili jambo pamoja na shamimu mmiliki wa blog ya 80/20 na Josephat Lukaza mmlimiki wa lukaza blog, wakati wa mkutano wa kuitambulisha VSOMO mfumo mpya unaomwezesha kijana wa kitanzania ,kupakua masomo ya ufundi stadi yanayotolewa na VETA kupitia simu yake ya Airtel
Baadhi ya bloggers wakipata futari
Baadhi ya wafanyakazi wa Airtel wakiwa kwenye Futari baada ya mkutano wa VSOMO.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...