Na Daudi Manongi-Dodoma
Waziri wa nchi na Ofisi ya makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe.January Makamba amesema kuwa wameandaa mashindano ya upandaji wa miti na ufufuaji visiki hai katika ngazi zote nchini ili kufanikisha mapinduzi ya kijani na kutoa kiasi cha pesa cha shilingi milioni 100 kwa halmshauri itakayofanya vizuri.

Waziri makamba ameyasema hayo alipokuwa akifunga warsha ya siku moja kwa wabunge kuhusu kukabiliana na tishio la jangwa na kuboresha ardhi iliyochakaa ili izalishe zaidi katika ukumbi wa Bunge wa Pius Msekwa jijini Dodoma.

Aidha amesema kuwa atashirikiana na Tamisemi na Wizara ya elimu kuhakikisha elimu ya upandaji miti na ufufuaji wa visiki hai inatolewa kuanzia ngazi ya elimu ya Awali ili wanafunzi waanze kupata elimu hii kuanzia katika ngazi ya chini.

Mhe.Mkamba alisema kuwa upandaji wa miti ndio utaleta manufaa makubwa nchini mwetu kwani hakuna sekta isiyotegemea miti toka uumbwaji wa dunia hii kwani Nyanja za Afya,ufugaji,misitu,utalii na maji zote zinategemea uhifadhi wa Mazingira yetu.

Aidha waziri huyo mwenye dhamana ya mazingira alisema kuwa kama jamii yetu haitahifadhi mazingira basi hakuna sekta itakayofaidika na kuongeza kwamba atasimama kidete kutengeneza mikakati ya maendeleo juu ya mazingira.Pia amehaidi Serikali kutenga fedha za kutosha,kutengeneza Sera nzuri,sheria na miongozo yenye tija katika mipango ya maendeleo.

Katika upande mwingine amesema kuwa kwa sasa utaratibu wa kufufua visiki hai ni jambo ambalo litawekwa katika mpango wa maendeleo ya Taifa na kuzitaka wizara zinazohusiana na mazingira kushirikisha watu wote ikiwemo kuwapa elimu kuhusu ufufuaji wa visiki hai.

Aidha Waziri Makamba amesema kuwa serikali ina mkakati mkubwa wa uboreshaji wa Sera za Mazingira uku mkakati wa kupanda na kutunza miti wa mwaka 2016-2021 ukiwa bado katika mipango mahususi ya kuifanya Tanzania kuwa ya Kijani.


Warsha hiyo kwa wabunge imeeandaliwa na shirika la Lead foundation uku ikishirikisha ofisi ya Bunge na wadau kutoka World Vision, Ever Green na World Agroforestry Center ambao walitoa mada mbalimbali kwa wabunge ikiwemo jinsi ya kuhifadhi Uoto wa Asili,Kilimo cha kijani,namna ambavyo ufufuaji wa Visika hai na Ngitili zinavyoweza kuchangia Mpango wa kitaifa wa Upandaji Miti na kuimarisha mshikamano kitaifa wa ustawishaji Miti.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 19, 2016

    Ni hatua nzuri lakini naona waziri analenga katika kumotivate na kuelimisha jamii,impact ya hili itachukua muda mrefu. kutokana na hali halisi ya nchi yetu kugeuka kuwa jangwa,serikali inapaswa kuchukua hatua za haraka,na zenye msukumo kulazimisha halmashauri zote kupanda,kukuza na kutunza miti.msukumo unaotakiwa unapaswa kuwa kama ule ambao serikali umechukua ktk kampeni za maabara kwa kila shule na madawati kwa kila mwanafunzi.

    ReplyDelete
    Replies
    1. AnonymousJune 20, 2016

      Naona km waziri amezungumzia hoja zako zote mbili 1:hatua ya haraka, halmashauri zipande miti na kutunza visiki hai, 2:Elimu -
      Elimu hapa inakuwa ni msingi sana kwa sababu suala la utunzaji mazingira lazima limuingie mtu na aelewe ukisema " utunzaji mazingira" una maanisha nini hasa. Mfano sijui km wengi wanaelimu ya utunzaji kisiki hai ambayo ni njia mojawapo ya utunzaji mazingira ambayo haihitaji rasilimali fedha kubwa.

      Delete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...