Ushirikiano wa karibu  wa mara kwa mara baina ya Vyama vya Wafanyakazi na Viongozi wa Taasisi za Umma  katika kutatua changamoto zinazowakabili Wafanyakazi  hasa maslahi yao ndio njia pekee inayosaidia kuwafanya watekeleze kazi zao kwa juhudi, maarifa na nidhamu.
Kauli hiyo imetolewa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi wakati akibadilishana mawazo na Uongozi Mpya wa Chama cha Wafanyakazi wa Sekta za huduma za Umma  (ZAPSWU)  uliofika kujitambulisha Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.
Balozi Seif Ali Iddi alisema ipo migogoro kadhaa inayowasumbuwa Wafanyakazi katika sekta tofauti Nchini na kuitanzua kwake ni kutafuta suluhu inayotoa fursa kwa kuwakutanisha wadau wote ili kupata njia ya kukabiliana na migogoro hiyo kwa njia ya mazungumzo ya amani.
Akifafanua mgogoro wa muda mrefu  uliowakumba wafanyakazi wa shamba la Mipira Kichwele dhidi ya mwekezji wa shamba hilo { Agro Tec } waliotaka kujua Viongozi hao wa Chama cha Wafanyakazi wa Sekta za Huduma za Umma Balozi Seif alisema Wizara ya Fedha na Uchumi ndio iliyopewa jukumu na Serikali Kuu kuangalia hatma ya suala hilo.
Balozi Seif alisema Wizara ya Fedha kwa sasa inaendelea kutafakari namna ya kuukwamua mradi huo kwa kutafuta mbinu nyengine za uwekezaji  baada ya kampuni iliyokodishwa kuendesha mradi huo  kushindwa kuliendeleza na kuwaacha wafanyakazi wake njia panda.
Mapema Katibu Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi  wa Sekta za Huduma za Umma Zanzibar { ZAPSWU } Bibi Mwatum Othman alisema Chama hicho kipya ni mjumuisho wa vyama vya Wafanyakazi vitatu vya Raaw, Zadgu na Zipau.
Bibi Mwatumi alisema Viongozi na wanachama wa vyama hivyo wamefikia muwafaka wa kuwa na nguvu za pamoja za kuunganisha vyama hivyo ili kupunguza utitiri wa vyama uliokosa uwakilishi madhubuti.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi wakati akibadilishana mawazo na Uongozi Mpya wa Chama cha Wafanyakazi wa Sekta za huduma za Umma ( ZAPSWU) uliofika kujitambulisha Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.
 Balozi Seif  akisisitiza jambo wakati wa mazungumzo yake na Uongozi wa Zapswu uliojumuisha wajumbe wa Baraza Kuu pamoja na Kamati Tendaji ya Chama hicho.
Kulia ya Balozi Seif ni Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Sekta za Huduma za Umma Nd.Ameir  Mwadini Nahoda.
Katibu Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi  wa Sekta za Huduma za Umma Zanzibar (ZAPSWU)  Bibi Mwatumu Othman akimuelezea Balozi Seif  hatua za kuunganishwa vyama vingi vya wafanyakazi na kupata kimoja chenye nguvu zaidi ya uwajibikaji.
Picha na OMPR,  ZNZ.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...