Aliyekuwa mbunge wa kwanza wa Ludewa Violeth Baraka (pichani) amefariki dunia jana katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam.
Taarifa kutoka kwa familia ya mbunge huyo zinadai kuwa kabla ya kifo chake mama Baraka alikuwa amelazwa katika Hospitali ya Muhimbili jijini Dar es Salaam na jana usiku alikutwa na mauti. mwili wake unategemewa kuzikwa kesho Ijuma jijini Dar es Salaam.
Marehemu Baraka alikuwa mbunge wa Ludewa kati ya mwaka 1965 hadi 1970. Na ndie mbunge wa kwanza kupigania Meli ya kwanza kufika katika Ziwa Nyasa meli ya MV Songea baada ya kilio cha wana Ludewa miaka hiyo. Meli iliwasili baada ya kulia na kutunga nyimbo kuwa wananchi wa Ludewa tunalilia Meli hiyo si tu kwa jimbo la Ludewa. Mama Baraka atakumbukwa si Ludewa pekee bali atakumbukwa kwa majimbo yote ya mwambao mwa ziwa Nyasa.
Mwenyezi Mungu ailaze
Roho yake mahali pepa peponi
Amen
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...