Na Bakari Madjeshi,
Globu ya Jamii.
Kituo Cha kusaidia Watu walioathirika na Dawa za Kulevya cha Life and Hope Sober House kilichopo Bagamoyo kimekanusha taarifa juu ya msanii wa miondoko ya Hip Hop, Rashid Makwiro, maarufu kama Chid Benz, kutoroka kituoni hapo.
Akikanusha tuhuma hizo za kutoroka kwa msanii huyo, mkuu wa Kituo hicho, Al-Kareem Bhanji ameiambia Globu ya Jamii kuwa Chid Benz aliondoka kituoni hapo baada ya kufuata taratibu zote za uongozi pale alipoonekana yuko sawa.
"Ukweli ni kwamba Chid hakutoroka kituoni hapo bali alifuata taratibu na baraka zote za uongozi zilizotolewa baada ya kuonekana yuko sawa"amesema Bhanji. Pia amekanusha taarifa ya kuwa Babu Tale alimtelekeza Chid kituoni hapo.
"Babu Tale alitoa ushirikiano wa hali ya juu katika kusaidiana kama mnavyojua ukweli mpaka kumleta Chid kituoni. Tulikuwa muda wote tunashirikiana naye" ameendelea kueleza Bhanji.

Mkuu wa kituo cha "Life and Sobber House Bagamoyo" Al-Karim Bhanj akizungumza na waandishi wa habari (hapo pichani) juu ya uvumi ulioenezwa kuwa Msanii Rashid Makwito al maarufu kwa jina la 'CHIDI BENZ' alitoroka kwenye kituo hicho cha kutibu waathirika wa Dawa za kulevya.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...