WANAFUNZI wa chuo cha kodi (TRA) waaswa kutoa elimu ya maswala mbalimbali ya kodi kwa vijana wenzao ili kujifunza na kukuza uelewa wa kulipa kodi kwa hiyari.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Elimu na Huduma kwa Mlipa Kodi TRA, Richard Kayombo wakati wa ufunguzi wa Jumuiya ya wanafunzi wa kodi vyuoni jijini Dar es Salaam leo. Amesema kuwa vijana wapewe elimu ya kulipa kodi kwa hiyari mapema ili kipindi watakapoanza kupata mapato waweze kulipa kodi bila kushurtishwa.

Amesema kuwa Jumuiya ya wanafunzi wa kodi vyuoni iliyofunguliwa leo iwe taa kwa jamii nzima na wanachama wa jumuiya hiyo waweze kutoa elimu ya kodi watakayoipata kwa wenzao ndani na nje ya mazingira ya chuo.


Mkurugenzi wa Elimu na Huduma kwa Mlipa Kodi TRA, Richard Kayombo akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa ufunguzi wa Jumuiya ya wanafunzi wa Kodi vyuoni katika chuo cha Kodi jijini Dar es Salaam.
Rais wa serikali ya wanafunzi wa chuo cha Kodi(TRA)-ITA, Juma Nadhiru (Aliyesimamama) akizungumza na wanafunzi wa chuo cha kodi wakati wa ufunguzi wa Jumuiya ya wanafunzi wa Kodi vyuoni katika chuo cha Kodi jijini Dar es Salaam leo, Pia amemshukuru mgeni rasmi kwa kufika katika chuo chao na kuwahamasisha wanafunzi wa chuo hicho kujifunza zaidi katika kuhamasisha jamii kulipa kodi kwa hiyari. Kaliokaa kutoka kushoto ni Mkuu wa huduma za wanafunzi  wa chuo cha kodi- ITA, Rashid Mzava, Mkurugenzi wa Elimu na Huduma kwa Mlipa Kodi wa TRA, Richard Kayombo , Meneja huduma kwa mlipa kodi wa TRA, Honesta Ndunguru na Afisa Huduma na Elimu kwa Mlipa kodi TRA, Julieth Shehiza.
 Wanafunzi wa chuo cha kodi(TRA) wakiwa katika ufunguzi wa Jumuiya ya wanafunzi wa Kodi vyuoni katika chuo cha Kodi jijini Dar es Salaam leo.
KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...