Mkuu wa Kituo cha Polisi Runzewe kilichopo Kata ya Uyovu wilayani Bukombe, Jackson Kirahuka akimuonyesha Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto aliyevaa koti) sehemu mbalimbali za kituo hicho ambacho Mbunge wa Jimbo la Bukombe, Dotto Biteko (katikati) aliuliza swali la nyongeza Bungeni hivi karibuni akisema kituo hicho kinahitaji matengenezo makubwa na kumuomba Naibu Waziri huyo kufanya ziara jimboni kwake kujionea kituo hicho. Hata hivyo, Masauni alisema Serikali yake itahakikisha kituo hicho kitakuwa katika hali nzuri. Aliyevaa Kaunda suti ni Mkuu wa Wilaya hiyo, Amani Mwenegoha. 

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na mamia ya wananchi wa Kijiji cha Nyakabale, Kata ya Mgusu, mkoani Geita ambao ni majirani wa Kampuni ya Uchimbaji wa Dhahabu ya GGM mkoani humo. Wananchi hao wamelalamika kuwepo na vitendo vya ukatili dhidi yao vinavyofanywa na baadhi wa askari wa kampuni hiyo. Hata hivyo Mhandisi Masauni aliwataka Polisi mkoani humo kufanya uchunguzi wa haraka dhidi ya tuhuma hizo.

Mkazi wa Kijiji cha Nyakabale, Kata ya Mgusu, mkoani Geita, Biosi Makongoro akitoa kero yake kwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,  Mhandisi Hamad Masauni (kushoto aliyekaa) dhidi ya Kampuni ya Uchimbaji wa Dhahabu ya GGM mkoani humo ambayo ipo jirani na kijiji hicho, kuwa askari wa kampuni hiyo wanadaiwa kuwanyanyasa wananchi hao wanapopita katika eneo la Kampuni hiyo. Hata hivyo Mhandisi Masauni aliwataka Polisi mkoani humo kufanya uchunguzi wa haraka dhidi ya tuhuma hizo.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia)  akiwasili Kituo cha Polisi Runzewe kilichopo Kata ya Uyovu wilayani Bukombe ambacho Mbunge wa Jimbo hilo, Dotto Biteko aliuliza swali la nyongeza Bungeni hivi karibuni akisema kituo hicho kinahitaji matengenezo makubwa na kumuomba Naibu Waziri huyo kufanya ziara jimboni kwake kujionea kituo hicho. Hata hivyo, Masauni alisema Serikali yake itahakikisha kituo hicho kitakuwa katika hali nzuri. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 11, 2016

    Yaani kweli kabisa Mh Mbunge umekwenda kulalamikia ubovu wa kituo Bungeni ukamtoa Naibu Waziri aje kutembelea Kituo cha Polisi kilichopo kwenye jimbo lako?? Kweli kabisa wewe kama Mbunge na wananchi wako wooooote na Serikali za mitaa mmeshindwa kukarabati hicho kituo wenyewe bila kulifanya kuwa jambo la kitaifa?? Yaani Kabisaa umekubali Mh Masauni achome mafuta kuja huko kwa kitu ambacho wewe, wananchi na Polisi Mkoa/ Wilaya mngeweza kukimaliza??

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...