SHIRIKA LA Majisafi na Majitaka Dar es salaam (DAWASCO), imetangaza kuwapo tatizo la upatikanaji wa huduma ya Maji katika maeneo yote yanayohudumiwa na mtambo wa Maji wa Ruvu Juu, jijini Dar es salaam, pamoja na maeneo yote ya mji wa Kibaha mkoani Pwani kutokana na mtambo huo kuzimwa kwa wastani wa saa 72, kuanzia siku ya Ijumaa 17/06/2016, Jumamosi 18/06/2016 na Jumapili 19/06/2016.
Akizungumzia kukosekana Kwa huduma hiyo ya Maji, Kaimu Meneja Uhusiano wa DAWASCO, Bi. Everlasting Lyaro, ameeleza  sababu ya kuzimwa kwa mtambo wa Ruvu Juu, ni kumruhusu Mkandarasi (WABAG) kuunganisha mtambo mpya wa Maji na ule wa zamani, ambapo baada kukamilika kwa kazi hiyo, uzalishaji wa Maji utaanza mara moja.“Tuko kwenye hatua ya mwisho ya kuunganisha mtambo mpya wa Maji na ule wa zamani, kazi hii ikikamilika, uzalishaji utapanda kutoka wastani wa lita Milioni 70 hadi kufikia lita Milioni 106 kwa siku hivyo kuweza kutimiza lengo letu la kumtua mama ndoo ya Maji kichwani” alisema Lyaro
Lyaro, ameeleza kuwa kuzimwa kwa mtambo huo, kutasababisha maeneo ya Mlandizi, Kibaha, Kibamba, Mbezi, Kimara, Ubungo, Kibangu, Makuburi pamoja na eneo lote la Tabata, Segerea hadi Kinyerezi kukosa huduma ya Maji.Hivyo, ametoa wito kwa wateja na wananchi wote kuhifadhi Maji ya kutosha na kuyatumia kwa matumizi muhimu na lazima ili kukidhi mahitaji yao kwa kipindi  chote cha kukosekana kwa huduma hiyo.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...