Mkuu wa Wilaya Iringa Mh Richard Kasesela ametoa rai kwa wananchi wa wilaya ya Iringa kuchangamkia fursa ya kilimo cha viazi vitamu. Alitoa rai hiyo katika siku ya Wakulima katika kijiji cha Luganga kata ya Ilolo Mpya tarafa ya Pawaga. 
Hafla hiyo iliyoandaliwa na mradi wa Viazi Lishe "Viable Sweet Potato Technlogies in Africa-VISTA na kufadhiriwa na seriakli ya watu wa Marekani (USAID) unajumuisha Halmashauri 7 ikiwemo IRinga, Wangingombe, Gairo, Mufindi, Ulanga,Mbozi na Chunya. 
Katika mradi huo wakulima wanahamasishwa kulima viazi lishe kwa ajili ya afya ya mama na mtoto na pia kwa ajili ya biashara ambapo bidhaa kama juice, chapati, kakau(clips), tambi, mkate , maandazi na bidhaa zingine nyingi huweza kutengenezwa ili kukuza kipato. 

Akimkaribisha mgeni rasmi Meneja wa Mradi wa VISTA Bwana Fred Grant alisema mradi huu uko katika mwaka wa 2 na ni wa miaka 3 ni muhimu Tanzania ikaanza kufikiria jinsi ya kuuendeleza nchi nzima kwani manufaa yake ni makubwa. Sherehe hizo pia zilihidhuriwa na waakilishi kutoka Halmashaurizote 7 zinazonufaika na mradi huo.
 Meneja mradi wa VISTA Fred Grant akiongea kumkaribisha Mgeni Rasmi Mh Richard Kasesela

 Mh Kasesela akifurahia Juice ya Viazi Vitamu na watoto Fabiana na Telephina wa Kijiji cha Luganga


Meneja Mkuu kiwanda cha Tosti ambao ndio wanunuzi wakubwa wa viazi akitoa melezo. Kiwanda hiki kipo Iringa na kina mahitaji ya viazi kiasi cha tani 150 kwa wiki za viazi mbalimbali.
 Mh Kasesela akifurahia kiazi kitamu

Mh Kasesela akifurahia Juice ya Viazi Vitamu na watoto

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...