Na Dac Popos, Globu ya Jamii.
Ni siku ambayo Brazil hawataisahau katika ulimwengu wa kandanda, ukiondoa kipigo cha 7-0 toka kwa Ujerumani kwenye kombe la dunia 2014. Wakicheza kandanda safi na kulishambulia lango la Peru kwa muda wote wa mchezo huku wakikosa nafasi nyingi za kutumbukiza mpira kimiani, mnamo dakika ya 77 Raul Riudiaz wa Peru anautumbukiza mpira wavuni kwa goli lenye utata na kuipatia Peru bao la kuongoza, mshika kibendera analikataa goli hilo, lakini baada ya mazungumzo kati ya waamuzi wote wanakubaliana kuwa ni goli na kupelekea majonzi mengine kwa Brazil.
Mpaka mwisho wa mchezo kwenye uwanja huo wa Gillette jijini Foxborough, Massachusetts nchini Marekani Brazil 0 Peru 1, na kuifanya Brazil kufunga vilago na kuyaanga mashindano hayo katika hatua ya mtoano.
Na katika uwanja wa Met Life, East Rutherford New Jersey, Equador iliivulumisha Haiti kwa mabao 4-0 na kukata tiketi ya robo fainali. Ingawa Haiti walimiliki mpira kwa asilimia 52 dhidi ya 48 za Equador lakini walijikuta wanafungwa mabao mawil kila kipindi.
Mabao ya Equador yalifungwa na Enne Valencia dakika ya 11,Jaime Ayovi dakika ya 20, Chriatian Nobor dakika ya 57 na Antonio Valencia dakika ya 78. Hivyo kwenye robo fainali Equador atapambana na Colombia, wakati Peru atakipiga Marekani.
Leo ni
MEXICO vs VENEZUELA
PARAGUAY vs JAMAICA




Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...