Hapa ilikua mwaka 1980 Muhammad Ali akiongea na waandishi wa habari katika uwanja wa ndege wa kimataifa Dar alipokuja Tanzania kushinikiza Tanzania isusie mashindano ya Olympic yaliyofanyika Urusi mjini Moscow. Pamoja na Tanzania kukataa shinikizo hilo, Muhammad Ali alipokelewa kwa heshima kubwa. Moja ya waandishi waliozungumza na Muhammad Ali alikuwepo Dr. Hamza Mwamoyo (wa tatu kushoto) ambaye kwa sasa ni mkuu wa idhaa ya Kiswahili ya sauti ya America (VOA) jijini Washington, DC.
Muhammad Ali akimbeba enzi hizo mtoto Iddi Alkhag akimtabiria kuwa atakua mpiganaji wa mchezo wa ngumi lakini katika kukua kwake Iddi Alkhag akaja kuwa  mchezaji wa mpira wa miguu anayechezea mpira wa kulipwa nchini Denmark. Wazazi wake mmoja ni Mtanzania ambaye ni Bahari Gangwe Khamisin Alkhag anayeishi Houston, Texas, nchini Marekani na mama ni Mdenmark.
Iddi Alkhag akiwajibika katika mpira wa kulipwa nchini Denmark
[DSC04402.JPG]
Hapa Iddi Alkhag akikabidhi jozi 20 za viatu ma shini gadi za mpira wa miguu kwa aliyekua katibu wa TFF Bwn. Frederick Mwakalebela, siku mchezaji huyo alipokanyaga ardhi ya Tanzania kwa mara yakwanza baada ya miaka 30 alipozaliwa nchini Denmark, kulia ni baba yake Khamsini Alkhag akiwa na mkewe mama wa mitindo Asya Idarous Khamsini (kushoto)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...