Mkuu wa Benki ya Kiislam ya KCB, Rashid Rashid, akizungumza wakati wa Kufuturu futari iliyoandaliwa na benki ya KCB iliyofanyika jijini Arusha Mwishoni Mwa wiki.
Baadhi ya wafanyakazi na viongozi pamoja na wateja wa benki ya KCB Arusha wakifuturu.
Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya KCB Tanzania, Moezz Mir, akizungumza wakati wa kufuturu jijini Arusha mwishoni mwa wiki.
KCB Tanzania imekuwa mwenyeji wa hafla ya futari kwa wateja na wadau wake wa jiji la Arusha. Shughuli hiyo ilifanyika katika hoteli ya kitalii ya Kibo Palace ambapo wageni zaidi ya mia moja walialikwa ili kushiriki pamoja futari katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani.
Mkurugenzi Mkuu wa benki hiyo Moezz Mir alipokuwa akikaribisha wageni wake alisema kuwa mwezi wa Ramadhani ni wakati muhimu wa kushiriki pamoja na kuendeleza umoja na amani nchini. “Nawashukuru wote kwa kuwa washirika wa muhimu sana kwa benki yetu ya KCB Tanzania. Tunathamini sana uhusiano wetu na nyie na kila mara tunaendelea kutafuta nafasi ya kuweza kuwapa huduma bora zaidi,” alisema Moezz.
KCB Tanzania ni benki ya kwanza nchini kwa kutoa huduma ya kibenki kwa kufuata masharti ya dini ya Kiislamu. Huduma hii ya kibenki inayofuata maadili ya Sharia hutolewa katika matawi yote ya KCB nchini hata hivyo benki ya KCB pia ina tawi maalum kwa huduma hii ambalo liko Lumumba jijini Dar es Salaam.
Katika bidhaa na huduma zinazotolewa chini ya Sharia ni pamoja na mikopo, uwekaji fedha na uwekezaji.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...