Na Zainab Nyamka,Globu ya Jamii

BEKI wa kulia aliyetia wino Yanga, Hassan Kessy pamoja na winga wa Coastal Union, Juma Mahadhi wameanza vizuri mazoezi yao baada ya kuonyesha uwezo wa hali ya juu huku kila mmoja akifunga goli katika mechi ya mazoezi waliyocheza kwenye uwanja wa Taifa,Jijini Dar es salaam.

Kessy ameanza mazoezi rasmi na Yanga baada ya kumaliza mkataba wake na wekundu wa Msimbazi na kujiunga nao huku wachezaji wa timu hiyo wakimpa sapoti kwa asilimia zote. 

Uwezo ambao kessy ameuonesha kwenye mazoezi hayo ni wa hali ya juu huku kwa mara kadhaa akimvisha kanzu Geofrey Mwashiuya aliyekuwa anakabana nae.

Naye Mahadhi ameonekana kuwa moto wa kuotea mbali ingawa mazingira halisi hakuwa ameyazoea ila ameweza kufunga goli moja kwa ustadi mkubwa sana na kocha mkuu wa timu hiyo Hans Van De Pluijm akisifia kiwango cha wachezaji wake hao wapya. 

Katika mazoezi hayo yaliyoanza saa kumi jioni yakiongozwa na mholanzi Hans Van De Pluijm akisaidiana na Juma Mwambusi yameshuhudiwa na mashabiki wa timu hiyo huku wakionekana kupiga makofi pale Kessy na Mahadhi wanapofanya vizuri uwanjani.

Baada ya kumalizika kwa mazoezi hayo mashabiki wameonekana kuwazonga Kessy na Mahadhi na kupiga nao picha wakiwapongeza kwa kazi nzuri waliyoifanya.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...