Rais wa kikundi cha Upendo Women's Group ambaye pia ndiye mwenyekiti cha kikundi hicho Mh:Theresia Greca,ametoa shukrani za dhati kabisa kwa Rais mstaafu wa Tanzania Mh: Benjamin William Mkapa kwa kuwachangia kikundi chao,Shukrani za pekee kwa Kaimu Balozi wa Tanzania Mrs Agnes Kayola na Ubalozi mzima kwa mchango wao mkubwa wa kufanikisha zoezi zima la ufanikishaji wa fedha za kuisaidia hospital ya Mwananyamala nchini Tanzania.{picha na maelezo toka Maganga One Blog}
Pichani wageni waalikwa kutoka sehemu mbalimbali waliohudhuria sherehe za uchangishaji wa fedha kwa ajili ya hospitali ya Mwananyamala ya jijini Dar es Salaam.Shukrani zinatolewa na wana Upendo Women's Group kwa ufanikishaji wa zoezi zima
Baadhi ya Viongozi na wanachama wa Upendo Women's Group,kina mama wenye makazi yao nchini Ubegiji wametoa shukrani zao za dhati kabisaa kwa kila mmoja alishiriki vyema katika kufanikisha shughuli yao ya uchangishaji wa fedha kwa ajili ya kuisadia hospitali ya Mwananyamala ya jijini Dar es Salaam nchini Tanzania.Wana Upendo wanapeleka shukrani zao kwa Rais Mstaafu Mh:Benjamin William Mkapa kwa kujitolea mchango wake,Bila kusahau shukrani zao kwa Kaimu Balozi wa Tanzania Mrs Agnes Kayola na Ubalozi mzima wa Tanzania nchini Ubelgiji.Wanatoa shukrani kwa vikundi mbalimbali vya maonyesho na kila mmoja aliyefanikisha zoezi zima.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...