Na Dac Popos, Globu ya Jamii.
Muda unazidi kutaradadi kuelekea mchezo wa nusu fainali ya kwanza ya michuano maalum ya Copa America kati ya wenyeji USA dhidi ya ARGENTINA. Mtanange huu utakaochukuwa nafasi ndani ya dimba la NRG Stadium, jijini Houston Texas, macho na masikio ya wengi yatakuwa ni kwa mchezaji bora mara 5 wa dunia, Lionel Messi.
Messi anategemewa kuongoza mashambulizi akizungukwa na Gonzalo Higuain, Aguerro, Erick Lamela na wengineo huku hali ya kiungo mshambuliaji Angel Di Maria akiwa kwenye hati hati ya kuukosa mpambano huu kutokana na majeraha.
USA itawakosa nyota wake kama Jermine Jones mwenye kadi nyekundu, Alejadro Bedoya na Bobby Wood wana kadi 2 za njano, wote hao walipata kadi hizo kwenye mchezo wa robo fainali dhidi ya Equador. Lakini tegemeo lao litabaki kwa mshambulizi Clint Dempsey ambaye amekuwa akifunga kwenye kila mchezo.
Swali kwa Kocha Jurgen Klinsmman atawatumia chipukizi Darlington Nagbe na Christian Pulisic au wakongwe Kyle Bekerman na Graham Zusi kuziba mapengo ya wachezaji watakaoukosa mchezo huu ili waweze kuutumia vizuri mfumo wa 4-3-3 ili kupata ushindi?
Muda ni ule ule wa kula daku ndipo tutakuwa tukiutazama mtanange huu.
Ni USA au ARGENTINA kwenda fainali sku ya jumapili tarehe 26/06/2016?




Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...