Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Mkazi imepata vifaa vya upimaji (Total Station) na kutegemea kupata mafunzo kuhusu matumizi yake kuanzia tarehe 13 Juni – 16 juni, 2016 kutoka nchini ya Korea ya Kusini.
Akikaribisha ujumbe wa wa-Korea hao Wizarani, Mkurugenzi wa Upimaji na Ramani, Bw. Justo Lyamuya amesema kuwa vifaa hivyo vya upimaji vitasaidia kuhuisha ramani zilizopitwa na wakati.
Bwn. Lyamuya ameelaza kuwa idadi ya vifaa vya upimaji vitakavyotolewa wakati wa mafunzo, vitakuwa vinne (4) – (Total Stations).
Kwa upande wake Munseok Lee, kiongozi wa ujumbe huo, amesema vifaa hivyo vilivyogharimu Dola 35,000 kila kimoja, vimenunuliwa Uingereza (UK – Datahawk) na kuwa vinauwezo wa kufanya kazi kwa masaa mia mbili (200) mfululizo, na kuchukua picha za angani kwa kila sekunde mbili, picha moja.
Aidha, Bwn. Lee alitoa ufafanuzi kwa vitendo kwa kifupi kuhusu matumizi ya kifaa hicho na kuahidi kutoa ufafanuzi wa kina zaidi kwa siku 4 (tarehe 13 – 16 juni), wakati wa mafunzo yatakayofanyika kwa Maafisa waliopo kwenye kada ya Upimaji na Ramani.
Vifaa hivyo vimetolewa na nchi ya Korea kwa nia ya kudumisha ushirikiano kati ya nchi ya Tanzania na Korea Kusini.
Munseok Lee, mtaalam wa upimaji, kiongozi wa ujumbe wa Korea, akionyesha sehemu inapokaa kamera katika kifaa cha upimaji (Total station) kwa Mkurugenzi wa Upimaji na Ramani, Justo Lyamuya na Mkurugenzi msaidizi wa Idara hiyo Elizabeth Mrema.
Jigez Kim, mtaalam wa upimaji kutoka Korea, akionyesha jinsi ya kufungua kifaa cha upimaji (Total station) katika Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, mbele ya Mkurugenzi wa Upimaji na Ramani, Justo Lyamuya (haonekani pichani).
Munseok Lee, mtaalam wa upimaji, kiongozi wa ujumbe wa Korea, akionesha kamera inayokaa ndani ya kifaa cha upimaji (Total station) na kuonyesha kwa Mkurugenzi wa Upimaji na Ramani, Justo Lyamuya na Mkurugenzi msaidizi wa Idara hiyo Elizabeth Mrema.
Mtaalam, Jigez Kim akionyesha jinsi ya kufunga parashuti hiyo kuirudisha ndani ya kifaa hicho cha Upimaji (Total station).
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...