Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
TIMU ya soka ya Vijana ya Shelisheli imeanza kujifua leo ikiwa ni maandalizi yake kuelekea Juni 26 katika mchezo wao dhidi ya Serengeti Boys ikiwa ni mechi ya kufuzu kucheza fainali za kombe la Mataifa Afrika kwa vijana nchini Madagascar chini ya miaka 17 unaotarajiwa kupigwa kwenye dimba la uwanja wa Taifa, Jijini Dar es Salaam.Timu hiyo imewasili leo alfajiri wakiwa na msafara wa watu 25 wakiwemo wachezaji pamoja na viongozi.

Mchezo huo utachezeshwa na waamuzi wanne kutoka nchini Ethiopi wakiongozwa na kamisaa wa mchezo huo anayetokea nchini Malawi. Kuelekea mchezo huo TFF imeshusha viingilio ili watanzania wengi kujitokeza kuipa hamasa timu yao katika mchezo huo muhimu.

Afisa habari wa TFF, Alfred Lucas amesema kuwa VIP B na C vitakuwa Sh. 5,000 huku mzunguko ukiwa Sh. 2000 na TFF imetoa tiketi 300 kwa vijana na shule za Makongo na Jitegemee ili kuwapa hamasa vijana wenzao kwani katika mpira shabiki ni mchezaji wa 12.

"TFF imetoa tiketi 3000 kwa wanafunzi wa Jitegemee na Makongo kwa ajili ya kuwapa hamasa vijana wenzao kwenye mchezo ambao ni muhimu sana ili kupata ushindi na hata hivyo pamoja na hilo tumeonelea kupunguza kiingilio kwa kuangalia hali za wananchi na kuweka kiasi ambapo kila mmoja atakizi,"amesema Alfred.

Kikosi hicho kitafanya mazoezi yake ya mwisho kesho kwenye uwanja Wa Taifa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...