Na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.
MAADHIMISHO ya wiki ya utumishi wa umma mwaka huu kufanyika kivingine ikitofautiana na miaka mingine yote ikiwa maadhimisho ya wiki ya utumishi wa umma hufanyika Juni 16-Juni 23 kila mwaka.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Manejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angela Kairuki wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Amesema kuwa watendaji wakuu katika wizara, Idara zinazojitegemea, Wakala na Taasisis za Serikali watatakiwa kutenga siku moja ya kukutana na watumishi wa umma katika sehemu zao za kazi kwaajili ya kusikiliza kero za watumishi wa umma kwa madhumuni ya kuzitafutia ufumbuzi pamoja na kutenga siku moja kwa watendaji wakuu kusikiliza kero za wananchi zinazohusiana na huduma zinazotolewa na taasisi zao na kuzitafutia ufumbuzi.

Pia amewaagiza makatibu wakuu, Katiu Tawala na mikoa na wakuu wa Taasisi za Umma na Mamlaka za Serikali za Mitaa wafanye Tathmini ya uwepo wa watumishi hewa na kutoa mapendekezo ya namna ya kuondoa changamoto hiyo.
Amesema kuwa kauli mbiu ya mwaka huu katika kuadhimisha wiki ya utumishi wa umma ni " Uongozi wa umma kwa ukuaji jumuishi kuelekea katika Afrika tunayoitaka."

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Manejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angela Kairuki akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo. kuhusiana na namna maadhimisho ya wiki ya utumishi wa umma yatakavyofanyika kwa mwaka huu.
 Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Manejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angela Kairuki jijini Dar es Salaam leo.
Picha na Emmanuel Massaka, Globu ya Jamii.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 11, 2016

    The mdudu, safi sana Tanzania mpya hiyo inakuja kwa kasi ya #AJABU

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...