Na Dac Popos, Globu ya Jamii.

Marekani imefanikiwa kuongoza kundi A mara baada ya kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Paraguay. Ikicheza mbele ya umati mkubwa wa mashabiki wake kwenye uwanja wa Lincoin Financial Field jijini Philadelphia, Marekani ilionyesha kiwango kizuri cha uchezaji na kunako dakika ya 27 Clint Dempsey aliifungia Marekani bao hilo pekee katika mtanange huo.

Ingawa Marekani walicheza pungufu ya mchezaji mmoja kwa muda mrefu wa mchezo, kwani dakika ya 36 beki wa kulia wa Marekani Yedlin alitolewa nje kwa kadi nyekundu baada ya kupata kadi ya pili ya njano, bado Marekani waliweza kulilinda lango lao na kushambulia kwa kushitukiza. Hadi mwisho Marekani 1, Paraguay 0.

Kwa kuongoza kundi kuna uwezekano mkubwa kuwa Marekani akawa amekwepa kukutana na Brazil katika hatua ya mtoano.
Kwenye mchezo kati ya Colombia na Costa Rica, kocha Jose Pekerman wa Colombia aliwapanga nyota wake kama wachezaji wa akiba kitu ambacho alikijutia baadaye, baada ya timu yake kupata kichapo cha mabao 3-2 toka kwa Cost Rica. 

Kituko au kivutio kwenye mchezo huu ilikuwa kwa mchezaji wa Colombia Frank Fabra, yeye alifunga mabao mawili, moja kwa kila timu yaani aliifungia timu yake dakika ya 7 na akaifungia timu pinzani (Costa Rica) dakika ya 34.

Mabao mengine ya Costa Rica yalifungwa na Johan Venegas dakika ya 2 na Celso Borges dakika ya 58. Na lingine la Colombia lilifungwa na Marlos Moreno.

Leo tutawashuhudia
HAITI vs EQUADOR
BRAZIL vs PERU

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...