Na Dac Popos, Globu ya Jamii.
Michuano ya Euro 2016 imeendelea jana kwa michezo mitatu kupigwa katika miji tofauti.
Kwenye dimba la Stade Bollaert-Delelis jijini Lens, Albania ikicheza na wachezaji kumi kwa muda mrefu wa mchezo ilichapwa bao 1-0 na Switzerland. Bao hilo pekee na la ushindi lilifungwa na Fabian Schar dakika ya 5 tu, kwa kichwa kufuatia mpira wa kona iliyopigwa na Xherdan Shaqiri, ambapo kipa wa Albania Etrit Berisha akipiga ngumi hewa kutaka kupangua mpira huo.
Kunako dakika ya 36 mwamuzi wa mechi hiyo Carlos Velasco Carballo wa Hispania alimwonesha kadi nyekundu nahodha wa Albania Lorik Cana baada ya kumpa kadi mbili za njano kwa kosa la kuushika mpira makusudi akimzuia Haris Seferovic asiende kufunga.
Katika dimba la Stade de Bordeaux, Gareth Bale mchezaji anayesukuma kandanda katika klabu ya Real Madrid aliiongoza Wales kuishinda timu ya Slovakia kwa mabao 2-1. Wales ambayo inacheza mashindano makubwa kwa mara ya kwanza tangia mwaka 1958 kwenye mashindano ya kombe la dunia, imerejea sasa na kucheza kabumbu safi.
Gareth Bale katika dakika ya 10 alipiga kwa ufundi mpira wa adhabu ndogo ambao ulikwenda moja kwa moja kimiani na kuiandikia Wales goli la kwanza ambalo lilidumu mpaka mapumziko.
Kunako dakika ya 61 kipindi hiki cha pili Slovakia walirejesha goli hilo kupitia kwa mchezaji Odren Duda.Lakini dakika ya 81 Wales walijihakikishia pointi tatu muhimu kwa kujipatia goli la pili lililofungwa na Hal Robson-Kanu.Hadi mwamuzi Sevein Oddvar Moen wa Norway anapuliza kipenga cha mwisho Wales 2,Slovakia 1.
Mchezo wa mwisho kwa usiku huo ambao ulikuwa unasubiriwa na wengi ni kati ya Uingereza na Urusi uliopigwa kwenye uwanja wa Stade Velodrome jijini Marseille.Kutokana na watu wengi kuifuatilia ligi kuu ya Uingereza basi wana hamu ya kuiona timu hiyo taifa inafanya nini kwenye michuano hii.
Mtanange huo ulikuwa mkali na wa kuvutia ni Uingereza ndiyo walifanikiwa kufika mara nyingi langoni mwa Urusi lakini washambuliaji wao wakiongozwa na nahodha Wayne Rooney, Adam Lallana, Harry Kane na wengineo hakuwa makini na kukosa nafasi nyingi za kujipatia mabao. Hivyo hadi mapumziko timu zote zikawa suluhu 0-0.
Kipindi cha pili kkunako dakika ya 56 'free kick' nzuri iliyopigwa na Eric Dier inazama nyavuni mwa Urusi na kuipatia Uingereza bao la utangulizi. Urusi nao hawakukata tamaa na juhudi zao zilizaa matunda kunako dakika ya 90 pale mabeki wa Uingereza Gary Cahill na Chris Smalling waliposhindwa kumzuia V.Berezutski kupiga kichwa mpira ulioenda moja kwa moja wavuni.
Leo ni vita kati ya
UTURUKI vs CROATIA......Uwanja: Parc de Prince
POLANDI vs IRELAND KASKAZINI....Stade de Nice
GERMANY vs UKRAINE......Stade Pierre Mauroy




Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...