Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
TIMU ya Mbeya City imeanza kuonesha mbwembwe za usajili baada ya kumpatia mkataba wa mwaka mmoja kiungo wa timu ya Prison, Mohamed Mkopi ambapo amesaini mkataba huo siku moja baada ya kujazwa fedha na Mdhamini wa timu hiyo kampuni ya Binslum.

Kampuni hiyo iliamua kuwaongezea mkataba wa miaka miwili ya udhamini  wa timu hiyo baada ya kuwa mabalozi wazuri wa bidhaa zao na hata baada ya kumalizika kwa ligi msimu uliopita, Mbeya City kupitia kwa mwalimu wake Kinnah Phiri wameweka wazi mipango yao kuelekea msimu ujao wa kusajili wachezaji wenye uwezo mkubwa ili kuisaidia timu hiyo.

Amesema, katika suala la usajili atahakikisha hafanyi makosa kwani lengo lake ni kuhakikisha msimu ujao timu inamaliza katika nafasi nzuri baada ya msimu uliomalizika wakimaliza nafasi ya nane wakiwa na alama 35 pia mwalimu huyo alimweka nyota wa Azam FC Didier Kavumbagu katika mipango yake kabla ya kutimkia nchini Vietnam kwa ajili ya shughuli zake za kisoka.

City walishaanza mazungumzo na Kavumbagu yaliyofikia katika hatua nzuri yalikuwa na lengo la kuimarisha safu ya ushambuliaji ya timu hiyo kutokana na kukabiliwa na tatizo la umaliziaji. Mbali na nyota huyo pia Phiri aliitisha mashindano mbalimbali ya vijana ili kusaka vipaji vipya vikavyoungana na nyota wengine na kuunda kikosi bora cha City.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...