Wakristu wapendwa,
Tumsifu Yesu Kristu.
Padre Peter Mushi na Padre Godfrey Amobi, wanapenda kuwatangazia ya kuwa, Misa yetu ya kiswahili itafanyika Jumapili tarehe 12 Mwezi Juni, 2016, Saa 8:00 mchana (Sunday 12, June 2016 at 2 pm). Tungeomba wakristu wote watanzania na Afrika ya Mashariki wajiunge nasi katika Misa hii. Na siku ya akina baba. Tunawakaribisha watu wote wanaopenda kuhudhuria ibada ya Kiswahili.
Anwani yetu ni: Kanisa la Mt. Cecilia,
120 East 106 Street,
New York, NY 10029.
Between Lexington and Park Avenue.
Chukua Train # 6. Mpaka kituo cha 110 St.
Halafu tembea ukirudi mpaka 106 St.
Ni matumaini yetu kwamba mtafika kwa wingi. Karibuni tumtukuze Muumba Wetu kwa lugha yetu ya Kiswahili.
Mbarikiwe. Kutoka kwa Padre Peter Mushi na Padre Godfrey Amobi
Karibuni...


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...