JUMUIYA YA WATANZANIA NORTHERN
 CALIFORNIA (TCO) JUNE 3 2016 TAMKO RASMI

Jumuiya yetu ya watanzania tuishio upande wa northern California,
Tunapenda kutoa tamko rasmi kwamba hatuhusiki na wala hatujahusishwa na hatutahusika kwa njia yoyote ile kushiriki kuweka sahihi zetu kwenye barua inayosemakana ipo na inahitaji sahihi za watanzania wanaoishi hapa ili kumlazimisha  au kumshinikiza Rais amuondoe Mh Balozi Masilingi.

Habari hizi zilitolewa juzi kwenye vikao vya bunge na Mh Joseph Mbilinyi alipokuwa akichangia kwenye hotuba ya waziri wa mambo ya nje. Pamoja na mengi mazuri aliyoyasema kuhusu diaspora lakini hili la kuishambulia ofisi ya ubalozi kutoshiriki na kutojali misiba ya watanzania wanaoishi USA, sio tamko letu sisi wanajumuiya na hatuhusuani na lawama hizi. Pili hili la kutaka kumuondoa Balozi Masilingi kwa nguvu nalo hatuhusiki na hatutausika kamwe. Tunatambua mchango mkubwa na ushirikiano mkubwa tunaoupata kutoka ubalozini.

Tunapenda kutoa ukumbusho kuwa sisi kama jumuiya hatujihusishi na siasa kabisa. Tunajihusisha na masuala ya kijamii katika mazingira tunayoishi na pia nyumbani.
Tunatoa pongezi kwa makundi na jumuiya nyingine za hapa usa walioliona hili na kulikemea hadharani.

Lakini pia jumuiya yetu haimzuii mtanzania yeyote miongoni mwetu kushirikishwa kwenye shughuli yoyote ile, ilimradi tu aifanye kwa utashi wake lakini si kwa jumuiya.

Asante
Erick Byorwango- Katibu mwenezi na mahusiano TCO.
Nakala: Ofisi ya ubalozi Washington DC.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...