Na Zainab Nyamka,Globu ya Jamii.
KIKOSI cha Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' Charles Boniface Mkwasa amekubali matokeo baad ya kufungwa goli 2 - 0 na Misri huku akisifia kikosi chao kuwa ni kizuri na wana wachezaji wazuri na wamecheza kwa nidhamu kubwa sana.

Akizungumza baada ya kumalizika kwa mchezo huo, Mkwasa amesema wachezaji wake wamecheza vizuri ila wameshindwa kutumia nafasi walizozipata katika kipindi cha kwanza na makosa madogomadogo kutoka kwa wachezaji na hasa ukiangalia goli la pili lilikuwa ni kosa la mabeki katika kufanya marking ya mwisho. Hata hivyo nawapongeza sana Misri kwani wamepata alama tatu na kuweza kufuzu Mataifa Afrika 2017 nchini Gabon.

"Wachezaji wamejituma sana na siwezi kuwalaumu kwani wamecheza na timu yenye uwezo mkubwa sana na wana wachezaji wa kimataifa wengi wanaocheza soka la kulipwa nje,"amesema Mkwasa.Baada ya matokeo hayo Stars wamesalia na pointi moja na Misri kujiongezea alama tatu na kufikisha saba ambazo zimempa nafasi ya kufuzu AFCON.
Benchi la ufundi la Taifa stars, Charles Boniface Mkwasa kushoto, Hemed Moroco kocha msaidizi Peter Manyika kocha wa makipa na Mkurugenzi wa Benchi la ufundi Abdala Kibadeniwa (kwanza kulia).


Mchezo ukiendelea jijini Dar es Salaam leo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 04, 2016

    Excuses excuses excuses.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 04, 2016

    Mboni hivi jamani?
    Walituambiaga kwamba timu haihitaji mzungu. Wakasemaga tutafute wachezaji vijijini afu wakae na Mswahili mwenzetu tuone kazi, ila kocha Mswahili alipwe mihela kaa kocha mzungu.
    Mboni kila siku tunakiona cha moto tu?

    ReplyDelete
  3. "Kufungwa twafungwa,! lakini chenga twawala" Ni yale yale mambo ya uswahili Swahili ambapo hatutaki kujifunza ipasavyo toka kwa wenzetu, eg Nigeria, Cameron,Ghana n.k.
    Labda Taifa Star kuna jipu linatakiwa kupasuliwa?

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 04, 2016

    Nafurahi kwa line ya benchi la ufundi.Benchi linauwezo mkubwa kiutaalamu wa soka na katika kujenga vipaji.Kuzidiwa katika mchezo ni kawaida.Matumaini bado yapo.tusonge mbele daima.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 05, 2016

    Wabongo si watu makini bali maneno mengi tu. Rais Kikwete alishughulikia mpira kwa nguvu zote akamleta kocha akawa anamlipa. Matokeo yake wabongo wakamfanyia fitina kubwa na majungu juu. Wakamwambia mzee wa watu Kikwete kuwa ana gudu������. Mpaka akaacha kwenda kuangalia mpira. Kelele na majigambo mengi lakini ni aibu tu ya watanzania.

    Timu hii imepata misaada sana. Mpaka wakawa wanakwenda kufanya mazoezi South Africa. Wakaenda kuweka kambi Uturuki...lakini kichwa cha mwenda wazima bhana. Ni bora sasa waachwe kwanza kupewa fedha ili hizo fedha zikafanye mambo ya maendeleo. Tumechoka sasa. Kila kitu hapa Tanzania ni unafiki na siasa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...