Mkuu wa Wilaya ya kinondoni, Salum Hapi akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya wananchi wa kinondoni kufuata sheria katika barabara ya mabasi yaendayo haraka.
Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.
Baadhi ya wananchi wakimsikiliza
Mkuu wa wilaya ya kinondoni,Salum Hapi amewataka wananchi wa kinondoni kufuata sheria katika barabara ya mabasi yaendayo haraka.
Hapi ameyasema hayo leo wakati akizungumza na waandishi juu ya utekelezaji wa agizo la Rais, amesema kuwa watu 49 wamekamatwa ambao wamekuwa wakitumia vyombo vya moto katika barabara ya mwendokasi
Hapi amesema kuwa barabara hiyo watu waheshimu sheria za nchi na watu watakaokiuka watachukuliwa hatua.
Aidha amewataka DART kuongeza ukaguzi wa abiria katika vituo vyake kwani sio watu wote wanasafiri wengine ni wahalifu,
Hapi amesema watu wote ambao wamekamatwa wafikishwa mahakamani kujibu mashitaka yao.





Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...