Kada wa Chadema na mbunge wa zamani wa Arumeru Magharibi, Goodluck Ole Medeye ametangaza leo rasmi kuhamia chama cha UDP.Ole Medeye amezungumza hayo mbele ya mkutano wa waandishi wa habari uliofanyika katika ofisi za Makao Makuu ya chama hicho,Mwananyamala jijini Dar.

Medeye amezungumza kwa kujipambanua kuwa yeye anasimamia haki na demokrasia, na kwamba amekerwa sana na tabia ya vyama vya Upinzani kutomheshimu Naibu Spika,Dkt. Tulia Ackson Mwansasu,pichani kati ni Mwenyekiti wa chama cha UDP,Mh.John Cheyo akishuhudia tukio hilo.
 Kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, Dkt.Goodluck Ole Medeye, akionesha kadi yake ya uanachama mbele ya Waandishir wa habari (hawapo pichani),kuashiria kuwa sasa ni mwanachama halali wa chama hicho cha United Democratic Party UDP,shoto ni Mwenyekiti wa chama hicho John Momose Cheyo.
  Dkt.Goodluck Ole Medeye, akikabidhiwa kadi ya uanachama mbele ya Waandishi wa habari (hawapo pichani) na Mwenyekiti wa chama hicho John Momose Cheyo.
Kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, aliyedumu na chama hicho kwa miezi kumi na moja Goodluck Ole Medeye, amekihama chama hicho na kujiunga na United Democratic Party UDP.

Bw. Medeye aliyewahi kuwa Mwanachama wa Chama cha Mapinduzi CCM na kuitumikia serikali katika nafasi ya Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, ametangaza uamuzi wa kuhama Chadema jijini Dar es Salaam na kukabidhiwa kadi ya UDP na Mwenyekiti wa Chama hicho John Momose Cheyo.

Mbunge huyo wa zamani wa jimbo la Arumeru Magharibi amejiunga na UDP akiwa na Mkewe, pamoja na watu wengine tisa wakiwemo waliokuwa kwenye vyama tofauti na wengine waliodai hawakuwahi kuwa kwenye siasa, ambapo katika maelezo yake, Ole Medeye amesema awali alitaka kuunda chama kipya lakini baada ya kupitia katiba za vyama akaona UDP ni sehemu sahihi.

Kuhusu masuala mbalimbali yanayoendelea nchini, wanasiasa hao wamelaani uminywaji wa demokrasia katika kipindi hiki, hususan ndani ya Bunge, na kushauri wabunge wa kambi ya upinzani wanaosusia vikao kurejea ndani ya ukumbi wa Bunge kwa vile njia wanayotumia haitabadili utaratibu wa kibunge hususan kumuondoa Naibu Spika kwenye kiti chake.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...