Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

Na Chalila la Kibuda, Globu ya Jamii
SERIKALI ya Mkoa wa Dar es Salaam, imeifutia  kibali kampuni ya Ukandarasi ya Ishinomya  cha  kufanya ujenzi wa  barabara za halmshauri zote za jiji la Dar es Salaam kutokana kujenga barabara chini ya kiwango huku kampuni tatu zimetakiwa zisipewe zabuni mpaka pale watakapojiridhisha.

Akizungumza na waandishi habari jijini  Dar es Salaam leo, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema kampuni zimekuwa ukandarasi zimekuwa zikifanya kazi chini ya kiwango ili barabara iharibike kwa ajili ya kupata zabuni nyingine.

Amesema kuwa hatuwezi kufika kwakuwa na barabara zenye kiwango cha chini  na kuendelea kuwepo kwa kampuni hizo ambazo zinajenga barabara chini ya kiwango na wanapofika mwisho nyuma zimeharibika.
Amesema kuwa mkoa wa Dar es Salaam barabara zina mashimo kutokana na kampuni kufanya kazi kwa mazoea.

Kampuni ambazo zimesimamishwa kufanya ukandarasi wa barabara mpaka wajiridhishe ni Germinex,  Delmonte  pamoja na Skol .
Aidha Mkuu wa Mkoa amewataka wakurugenzi wa halmashauri zote za Mkoa wa Dar es Salaam ndani ya mwezi mmoja kuwe hakuna barabara inayokuwa na mashimo na ni agizo  ambalo wanatakiwa kutekeleza.   

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. My humble best wishes goes to you Hin Makonda and we are behind your shoulder and toes \


    watakuelewa tu

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 24, 2016

    Kwa hili nakuunga mkono mh RC. Keep up the good work sir

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...