Mratibu wa Masoko na Msamizi wa Mauzo wa Shirika la ndege la Etihad nchini Tanzania, Grace Festo Kijo akiwakaribisha wageni mbalimbali wakiwamo wateja, mawakala na wadau mbalimbali wa shirika la ndege la Etihad katika futari maalum iliyoandaliwa na shirika hilo mwishoni wa juma katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam.)
Mratibu wa Masoko na Msamizi wa mauzo wa Shirika la ndege la Etihad nchini Tanzania, Grace Festo Kijo (wa pili toka kushoto) akibadilishana mawazo na wadau mbalimbali wa shirika la ndege la Etihad katika hafla ya futari maalum iliyoandaliwa na shirika hilo mwishoni wa juma katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam.
(Kutoka kushoto) Bw. Naeem Razzaq na Ifnan Aslam kutoka Kampuni ya TT Worlwide wakiwa pamoja na Meneja wa Marmara Travel services Bw. Talib S. Talib katika hafla ya futari maalumu kwa wateja, mawakala na wadau wa Shirika la ndege la Etihad iliyofanyika katika hoteli ya Serena wiki iliyopita.
(Kutoka kushoto) Bi. Glory Msangi wa Travel link , Mkurugenzi wa Traveluxe Africa Bw. Azhar Rajan , Mkurugenzi Mtendaji Travel link Ephrem T. Mtuya na Mkurugenzi Mtendaji Sophy travel & Tourism Safia Mnyema wakigonganisha glass wakati wa hafla ya kupata futari maalumu iliyoandaliwa na Shirika la Ndege la Etihad kwa wateja, mawakala na wadau wa Shirika hilo iliyofanyika katika hoteli ya Serena mwishoni mwa juma.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...