Shirika la Maji Safi na Majitaka Dar-es-salaam (DAWASCO), linawatangazia  wakazi wa jiji la Dar-es-salaam na  Mji wa Kibaha mkoani pwani kuwa Mtambo wa kuzalisha Maji wa Ruvu Juu utazimwa kwa wastani wa Saa 72, kuanzia siku ya Ijumaa 17/06/2016, Jumamosi 18/06/2016 na Jumapili 19/01/2016.

Sababu ya kuzimwa kwa Mtambo wa Ruvu Juu ni kumruhusu Mkandarasi (WABAG) kuunganisha mtambo mpya wa Maji na ule wa zamani. Kazi hii ikikamilika, uzalishaji unategemea kuanza mara moja, hivyo kumtua mama wa Dar es salaam ndoo Kichwani.

Kuzimwa Kwa mtambo wa Ruvu Juu kutapelekea maeneo yafuatayo kukosa Maji:
MLANDIZI, KIBAHA, KIBAMBA, MBEZI, KIMARA, UBUNGO, KIBANGU, MAKUBURI PAMOJA NA ENEO LOTE LA TABATA, SEGEREA HADI KINYEREZI.

WANANCHI MNASHAURIWA KUHIFADHI MAJI NA KUYATUMIA KWA MATUMIZI YA LAZIMA
DAWASCO INAOMBA RADHI WANANCHI WA MAENEO HUSIKA KWA USUMBUFU UTAKAOJITOKEZA.
Kwa taarifa zaidi wasiliana nasi kupitia kituo cha huduma kwa wateja 022-2194800 au 0800110064 (BURE).

IMETOLEWA NA:
OFISI YA UHUSIANO
DAWASCO-MAKAO MAKUU

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...