Katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii nchini Maj. Gen. Gaudence Milanzi amesisitiza
kuwa Tanzania ndio nchi pekee Duniani yenye ukweli wa kisayansi
unaothibitisha kuwa ndipo binadamu wa kwanza alipo patikana na kuanza
kusambaa maeneo mengine Duniani na si kama baadhi ya nchi zinavyo jitangazia
kuwa uridhi huu wa kihistoria ni wao.
Ameyasema haya kati ufunguzi wa Onesho kubwa la Kihistoria lililopo
Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni lenye kuonesha ukweli huu wa
kisayansi uliotokana na Tafiti mbali mbali zilizo fanywa na watafiti Duniani kama
ule wa Laetoli mwaka 1978 na mtafiti Dkt. Mary D. Leakey zinazo onesha nyayo
ziliachwa na zamadamu anayeiitwa Australopithecus afarensis na ni ushaidi
usiopingika wa zamadamu kutembea wima kwa miguu miwili takribani miaka milioni
3.6 iliyopia.
Akizungumza katika ufunguzi wa Onesho hilo kwaniaba ya Balozi wa Spain nchini
Msaidizi wa Balozi wa Spain nchini Bw Guilaume M. Juarez alisema kuwa
binadamu wote tunapaswa kuheshimiana kama ndugu kwani tafiti nyingi Duniani
zinadhihirisha ukweli usiopingika kuwa binadamu wote duniani wametoka Afrika na
ni Tanzania hivyo watu wote ni watanzania.
Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Prof Audax Mabula na Mwenyekiti wa
Bodi ya Shirika la Makumbusho ya Taifa Bi Anna Abdala, wametoa wito kwa
watanzania wote hususani waliopo jijini Dar es Salaam hasa wazazi na watoto
kuitembelea Makumbusho hiyo kwa lengo la kujifunza uwalisia wa ubinadamu wao
badala ya kutumia muda mwingi kwenye sehemu zingine za starehee.
Onesho hilo la Chimbuko la Mwanadamu lililopo Makumbusho na Nyumba ya
Utamaduni Dar es Salaam, Mtaa wa Shaban Robart mkabala na chuo cha
Usimamizi wa Fedha IFM sambamba na maonesho mengine litakuwa wazi kuazia
saa tatu asubuhi na kufungwa saa 12 jioni kila siku za Juma.
Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii katikati Maj. Gen. Gaudence Milanzi
akita utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa Onesho la Historia ya Chimbuko la
Mwanadam lililopo Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni DSM. Wanao
shuhudia kuliani Mwenyekiti wa Bodi ya Makumbusho ya Taifa Mh Anna Abdala
na kushoto ni mwakilishi wa Balozi wa Spain nchini Bw Bw Guilaume M. Juarez ,
Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Prof Audax Mabula na Mkurugenzi
wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dsm Bw Achiles Bufure.
Katibu Mkuu wa Waizara ya Maliasili na Utalii Maj. Gen. Gaudence Milanzi na
wageni wengine wakipata maelezo ya historia ya chimbuko la Mwanadamu
kutoka kwa Maratibu wa Onesho hilo Dr Agnes Gidna.
Mwenyekiti wa Bodi ya Makumbusho ya Taifa Mh Anna Abdalla akilitazama moja
ya fufu la Binadamu wa kale wanaosadikiwa waliishi takribani miaka Milioni 3.6
iliyopita.
Katibu Mkuu wa Waizara ya Maliasili na Utalii Maj. Gen. Gaudence Milanzi na
wageni wengine wakipata maelezo ya historia ya chimbuko la Mwanadamu
kutoka kwa Maratibu wa Onesho hilo Dr Agnes Gidna.
Katibu Mkuu wa Waizara ya Maliasili na Utalii Maj. Gen. Gaudence Milanzi na
mwakilishi wa Balozi wa Spain nchini Bw Bw Guilaume M. Juarez wakiangalia kwa
umakini mkubwa masalia ya wanyama wakale walioishi trakribani miaka Milioni 4
iliyopita.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...