Balozi wa Tanzania Nchini Nigeria, Balozi Daniel Ole Njolaay akimkabidhi hundi ya dola 2000 za Kimarekani sawa na kiasi cha zaidi ya shilingi milioni nne, Mh. Dk Angelina Mabula, Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za Rais Dk. John Pombe Magufuli katika kuhakikisha shule za msingi zinakuwa na madawati ya kutosha hapa nchini, Hafla hiyo ilifanyika kwenye ubalozi wa Tanzania jijini Abuja nchini Nigeria mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa Maendeleo ya Makazi jijini humo.
Mh. Dk Angelina Mabula Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makaziakizungumza katika hafla hiyo huku Balozi Daniel Ole Njolaay akimsikiliza.
Mh. Dk Angelina Mabula Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazipamoja na Balozi wa Tanzania nchini Nigeria Balozi Daniel Ole Njolaay wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya maofisa wa ubalizi huo na Shirika la Nyumba la Taifa NHC.
Mh. Dk Angelina Mabula Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Balozi Daniel Ole Njolaay pamoja na maofisa waubalozi huo na Shirika la Nyumba Tanzania NHC wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya hafla hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 09, 2016

    Tunashukuru juhudi hizi za kuchangia maendeleo ya vifaa muhimu vya shule. Shule ziwe na utaratibu na fungu la kuita maseremala kuhakikisha matengezo ya madawati pale yanapotakiwa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...