• Simu za Bure zinapatikana katika maduka yote ya Airtel
              •Utapata vifurushi vinavyodumu kwa muda wa miezi minne na muda                       wa maongezi zaidi ya dakika1000

Kufuatia tamko la serikali la kuzima simu zote bandia ifikapo tarehe 16 Juni 2016, Airtel Tanzania imeanzisha ofa kabambe ya “simu za bure na halisi" zinazopatikana katika maduka yote ya Airtel. Tangazo hilo limesema kwamba simu za Bure na halisi zinapataikana kwa wateja wote wenye simu bandia na  ambazo sio za viwango vinavyokubalika  katika soko la Tanzania  , kwa kununua kifurushi chenye dhamani  ya sh. 22,000 / = Tshs tu.   Simu hizi za bure na halisi zinazotolewa  na Airtel ikiwemo  ITEL 2090 na FERO 180, zikiwa na dakika  550  kwa kupiga mitandao yote, zenye ujumbe mfupi 3000 na 250 MB kwa muda wa miezi minne.
 Akitoa maoni yake juu ya ofa hii, mkuu wa kitengo cha  Internet Airtel Tanzania, Gaurav Dhingra alisema "tunatambua kwamba baadhi ya wateja wetu  bado wanatumia simu ambazo hazina uhalisia, hivyo wako katika hatari ya kuzimiwa simu zao hapo itakapofika siku ya Alhamisi, Juni 16.  Tunachukua fursa hii kuwahakikishi wateja wetu kuwa simu zao zitazimwa lakini laini zao hazitahadhirika  na katika kuwasaidia wateja kuweza  kununua simu zenye kiwango kinachokubalika, tumeamua kutoa simu zenye uhalisi bure pindi mteja atakaponunua kifurushi kitakachodumu kwa muda wa mienzi 4
 Dhingra aliendelea kufafanua kuwa, ili kuwapa wateja wetu uwezo wa kuchagua simu zinazokidhi mahitaji yao ,  tumeongeza simu za aina mbalimbali ikiwemo Magnus Z11, Huawei Y3C na Techno W3  ambapo mteja akinunua anapata kifurushi chenye dakika zaidi ya 1000 . "Tunatoa wito kwa wateja wetu wa Airtel wenye simu bandia kufika kwenye duka letu lolote la Airtel na simu yake ili ajipatie  simu yenye kiwango kinachokubalika kwa gharama nafuu zaidi kwa kununua kifurushi cha Airtel na kupata simu bure. "alinukuliwa Dhingra
Wateja wa Airtel wanaweza kuhakikisha kama simu zao ni bandia au la, kwa kupiga *#06# au kutembelea mawakala katika maduka ya Airtel lililokaribu nae.
Mkuu wa kitengo cha Internet Airtel Gaurav Dhingra akionyesha simu zinazopatikana kwenye maduka yote ya Airtel katika ofa iliyozinduliwa hivi karibuni kufuatia tamko la serekali la kuzima simu zote bandia ifikapo tarehe 16 Juni 2016. Simu hizo zinauzwa kwa gharama nafuu kabisa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...