Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
ZIKIWA zimesalia siku kadhaa kuelekea kwenye mtanane unaisubiriwa kwa hamu na mashabiki wa Yanga dhidi ya TP Mazembe unaotarajiwa kupigwa Juni 28, huku Yanga wakiwa kambini nchini Uturuki Meneja Yanga Hafidh Saleh amesema kuwa kikosi kinaendelea vizuri na zaidi hali za wachezaji wote wapo kwenye hali nzuri na tayario Oscar Joshua ameshaanza mazoezi na wenzake.

Salehe amesema kuwa wachezaji wanaendelea na mzoezi jioni ya leo katika viwanja vya hoteli ya Rio katika jiji la Antalya huku wakionekanakuwa na morali ya hali juu na wamehakikishia kuwa watafanya vizuri katika mchezo wao huo na zaidi watakuwa kwenye uwanja wa  nyumbani.

“wachezaji wapo kwenye hali nzuri na hata Oscar ameshaanza mazoezi na wenzake na zaidi wameonyesha morali ya hali ya juu kuelekea mchezo huo na wamehakikishia benchi la ufundi kuwa watatoka na ushindi hasa baada ya makosa yaliyojitokeza na kupoteza mechi ya kwanza dhidi ya Mo Bejaia,”amesema Saleh. Mbali na hao pia hali ya Nadir Haroub ‘Canavaro’ na Said Makapu wanaendelea  vizuri kwani walikuwa kidogo wanaumwa na watajumuika na wenzao jioni kwa ajili ya mazoezi.

Naye Mkuu wa Kitengo cha Habari wa Yanga, Jerry Muro amesema kuwa kutokana na uchakavu wa jenereta na kutokuwa kwenye hali nzuri ya kutumika wameamua mechi yao dhidi ya TP Mazembe sasa itapigwa majira ya saa kumi Jioni.

“Mechi itachezwa saa kumi jioni hasa baada ya jenereta la uwanja kutokuwa na uwezo wa kufanya kazi vizuri kutokana na uchakavu wake kwahiyo mashabiki wa Yanga na wanachama wajitokeze kwa winio kuja kuishangilia timu yao kwa morali kubwa na kuipa sapoti dakika zote 90, amesema Muro.”

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...