Wanafunzi kutoka vyuo vikuu vya Tanzania wanaochukua fani ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) wakionyesha vyeti vyao mara baada ya kumaliza programu ya wiki tatu ya“Seeds for the future” ambayo ilifanyika katika makao makuu ya Huawei Technologies yaliyopo Shenzhen, China. Programu hiyo inaendeshwa na kudhaminiwa na Kampuni ya mawasiliano na teknolojia, Huawei Tanzania.
Wanafunzi kutoka vyuo vikuu nchini Tanzania wanaochukua fani ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) wakizungumza na Balozi wa Tanzania nchini China Mhe. Lt. generali (Mstaafu) Abdulrahaman A. Shimbo katika ufunguzi rasmi wa programu ya “Seeds for the future” ambapo wanafunzi 10 kutoka Tanzania walipata fursa ya kujifunza kwa vitendo juu ya fani hiyo ya teknolojia na mawasiliano kwa muda wa wiki tatu, programu iliyodhaminiwa na kampuni ya mawasiliano na teknolojia, Huawei Tanzania.
Wanafunzi 10 kutoka vyuo vikuu vya hapa nchini wanaochukua fani ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) wakiwa katika picha ya pamoja walipotembelea sehemu ya makumbusho katika mji wa Shenzhen nchini China walipokuwa nchini humo kushiriki mafunzo kwa vitendo kupitia programu ya Seeds for the Future” inayoendeshwa na kudhaminiwa na kampuni ya mawasiliano na teknolojia, Huawei Tanzania.
Shenzhen, China. 08 Juni 2016. Wanafunzi kutoka vyuo vikuu vya hapa nchini ambao walikwenda China kuhudhuria mafunzo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), wameipongeza Kampuni ya Huawei Tanzania kwa kuanzisha mradi huo wenye lengo la kuongeza ufanisi kwenye masuala ya TEHAMA nchini na kuongeza uelewa juu ya katika sekta ya mawasilino na kuhamasiha ushiriki wa kimataifa katika Teknolojia ya habari na mawasiliano.
Wakizungumza wakati wa mahafali baada ya mafunzo ya programu ya Seeds fo the Future" katika makao makuu ya Huawei Shenzhen nchini China, walisema wanatambua mchango mkubwa unaotolewa na Huawei ili kuleta maendeleo katika sekta ya teknolojia ya habari na mawasiliano nchini Tanzania.





Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...