Serikali imewataka watumishi wa umma mkoani Ruvuma kutimiza kikamilifu wajibu wao ndipo wadai haki wanazostahili

Rai hiyo imetolewa leo na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Songea Benson Mpesya wakati alipozungumza na watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na wilaya ya Songea kwenye ukumbi wa Maliasili mjini Songea .Ameyasema haya ikiwa ni utekelezaji wa maadhimisho ya wiki ya utumishi wa umma ambapo viongozi na watendaji wakuu wa taasisi za umma wanakutana na watumishi wao kusikiliza kero na changamoto zinazokwamisha utendaji kazi

Mpesya amewataka watumishi wa serikali kutafakari kwa makini majukumu yao na huduma yao kwa umma kama inakidhi viwango vinavyotakiwa na wananchi na hivyo kustahili malipo.Aliongeza kusema watumishi wanao wajibu kwa umma wa kuwahudumia kwa weledi,wakati na bila ubaguzi wa dini au kabila au eneo analotoka mtu

Amekemea tabia ya baadhi ya watumishi wa serikali kudai haki na marupurupu bila kutimiza wajibu wao.Kila mtumishi anatakiwa kujua wajibu wake ndani ya ofisi anayoifanyia na ndipo haki zake zitafuata kwa mujibu wa sheria ,kanuni na taratibu za utumishi wa umma.

“Mnatakiwa kutambua kuwa ninyi watumishi wa serikali ni watoa huduma mlioajiliwa na wananchi wa Tanzania hivyo muwaheshimu na kuwathamni” alisema Mpesya.Amewonya watumishi wa umma kutokufanya kazi kama wanaharakati na walalamikaji badala yake watumie taaluma zao kutekeleza kazi zao

“Taifa letu linakwenda pabaya kwani tumekuwa na watumishi wa umma wanaofanya kazi ya kuorodhesha kero na changamoto badala ya kusaidia kutatua na kuwahudumia wananchi kuyafikia maendeleo wanayoyahitaji” alisema Mpesya.Hivyo amesisitiza watumishi wote kutumia weledi wa taaluma zao na kujiamini wakati wote wanapotekelza kazi zao huku wakiacha tabia ya kuwasumbua wananchi kwa kuwaeleza njoo kesho 

Pamoja na changamoto wanazokutana nazo watumishi wa umma Mpesya amewetakawa kuwa wakweli na kuepuka lugha ya njoo kesho ambazo ni lugha za kisiasa.
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma ambaye pia ni mkuu wa wilaya ya Songea Benson Mpesya akiongea na watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma na wale wa Ofisi yake leo ikiwa ni utekelezaji wa Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma ambapo viongozi na watumishi wanakutana kujadili na kutatua kero mbalimbali.
Sehemu wa watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma wakiwa kwenye kikao kazi cha kujadili kero na changamoto za utendaji wao ikiwa ni wiki ya maadhimisho ya utumishi wa umma.Kikao kimefanyika katika ukumbi wa Maliasili uliopo ofisi ya Mkuu wa Mkoa leo.
Afisa Utumishi katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Ruvuma Happy Msanga akitoa maelezo kwa mgeni rasmi kuhusu namna ambavyo Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yalivyotelezwa.Wa kwanza kulia ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Benson Mpesya na kushoto ni Kaimu Katibu Tawala Mkoa Joel Mbewa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...