Na Sultani Kipingo
Mchakato wa uchaguzi mkuu wa klabu Dar es salaam Young Africans Football Club maarufu kama  Yanga  ulifanyika kwa utulivu na amani na kumalizika salama jana Jumamosi katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salam na matokeo kamili ni  kama ifuatavyo:
Mwenyekiti Yusuph Manji (pichani juu) alitangazwa mshindi rasmi wa kiti hicho kwa mara ingine tena baada  kuzoa kura zote za ndio isipokuwa mbili tu. Yaani alipata  kura 1,468 kati ya 1,470 zilizopigwa huku kura mbili tu zikiharibika. Hakukuwa na kura ya hapana. Manji hakuwa na mpizani kwenye nafasi hiyo.
Makamu mwenyekiti Clement Sanga ambaye naye pia alikuwa akigombea  nafasi hiyo kwa mara ingine kwa kupambana  na Titus Osoro, aliibuka mshindi  kwa  kujizolea kura 1,428 kati ya 1,508 zilizopigwa. Mpinzani wake aliambulia kura 80 tu.
Nafasi za 20 za ujumbe ambazo wagombea waliibuka na ushindi katika uchaguzi huo ni:
1. Siza Augustino Lymo (1027)
2. Omary Said Amir (1069)
3. Tobias Lingalangala (889)
4. Salim Mkemi (894)
5. Ayoub Nyenzi (889)
6. Samuel Lucumay (818)
7. Hashim Abdallah (727)
8. Hussein Nyika (770)
Idadi ya wajumbe 12 ambao walishindwa kuibuka na ushindi baada ya kura kutotosha ni: 
1. David Luhago (582)
2. Godfrey Mheluka (430)
3. Ramadhani Kampira (182)
4. Edgar Chibura (72)
5. Mchafu Chakoma (69)
6. George Manyama (249)
7. Bakari Malima "Jembe Ulaya" (577)
8. Lameck Nyambaya (655)
9. Beda Tindwa (452)
10. Athumani Kihamia (558)
11. Pascal Lizer (178)
12. Silvester Haule (197)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...