
AROBAINI.
Familia ya Marehemu Mzee Gaspar Mtonga wa Majumba Sita Ukonga Dar es Salaam inayoheshima kuwakaribisha ndugu, jamaa na marafiki zetu wote kwenye Arobaini ya baba yetu mpendwa MZEE GASPAR MTONGA itakayofanyika Kijijini kwetu Mwangaza Matombo Morogoro leo tarehe 15 Julai, 2016 kuamkia kesho tarehe 16 Julai, 2016.
Shughuli hii itatanguliwa na Mkesha ambao utakuwa leo tarehe 15 Julai, 2016 na kufuatiwa na Ibada itakayofanyika kesho saa tatu asubuhi katika Kanisa katoliki la Mt. Paulo Matombo Morogoro ambapo pia zitafuatiwa na shughuli za kupanda Msalaba na hatimaye kuhitimishwa kwa Sadaka ya Chakula cha mchana nyumbani Kijijini Mwangaza Matombo Morogoro.
Tunawashukuru Sana. Mungu Awabariki.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...