Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo (kulia) akimkadhi cheti Kaimu Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Fadhil Bushagama, tuzo ya mshindi wa pili katika sekta ya mabenki baada ya benki hiyo kuonyesha ubora na ufanisi katika kutoa huduma za kibenki, tuzo hiyo imetolewa na Tan Trade kwenye maonesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Fadhil Bushagama akipeana mkono na viongozi baada ya kupokea tuzo.
Baadhi ya washiriki wa hafla ya utoaji tuzo kwa makampuni na taasisi zilizofanya vizuri katika Maonesho ya Sabasaba. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Fadhil Bushagama.
Meneja wa Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Fadhil Bushagama (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na maofisa wa Benki hiyo, Kilo Mgaya (kushoto), Willy Kamwela, baada kupokea tuzo ya mshindi wa pili katika sekta ya mabenki baada ya benki hiyo kuonyesha ubora na ufanisi katika kutoa huduma za kibenki, tuzo hiyo imetolewa na Tan Trade kwenye Maonesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa jijini Dar es Salaam.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...