Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya DCB, Edmund Mkwawa akizungumza na waandishi habari juu ya huduma zinazotolewa na benki hiyo katika maonesho ya biashara ya Kimataifa katika viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya wananchi wakipata huduma katika moja ya banda la DCB katika maonesho ya biashara ya Kimataifa katika viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.
MKURUGENZI Mtendaji wa Benki ya DCB, Edmund Mkwawa amesema kuwa benki imejikita katika kuinua uchumi kwa wananchi.
Akizungumza na waandishi habari wakati maonesho ya Kimataifa ya katika viwanja vya Mwalimu Nyerere, Mkwawa amesema tangu kuanzishwa kwa benki hiyo wameweza kutoa mikopo zaidi ya watu 4000 wanaojishughulisha na ujasirimali.
Mkwawa amesema kuwa benki imekuwa ifanya huduma mbalimbali pamoja na kuhudumia halmashauri za jiji la Dar es Salaam katika kuhakikisha wananchi wanakuwa kiuchumi kwa kuwapa mikopo yenye riba nafuu.
Amesema kuwa DCB ni benki iliyoanzishwa na wazalendo ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za kibenki tofauti na benki zingine kutokana na ripa inayotolewa na benki hiyo.
Aidha amesema kuwa benki hiyo imekuwa ikikua kwa kasi kwani hadi sasa imefikisha matawi 10 na mawakala wanaofanya kazi na benki hoyo katika kutoa huduma ni zaidi ya 1000.
Mkwawa amesema kuwa wana maombi ya mikopo kwa wajasiriamali ili kuweza kukua kiuchumi pamoja na kutanua biashara zao.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...